Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2000, wakati huo naishi na mjombangu hapa Dar. Nilikuwa nimepata kibarua pale karibu na Tazara. Nilikuwa nimemaliza darasa la Saba kijijini na kukaa kwa miaka mitatu, kabla hajaagiza niletwe mjini.
Mwaka huo wa 200 nilikuwa na miaka miwili tangu kutoka kijijin. Kwa kupata kibarua na kwa vile mjomba ni mtu anayefahamika kidogo kutokana na kuwa nazo kiasi, nilikuwa mtu wa kujikweza nakujiona babu kubwa.
Hata pale kwa familia ya mjomba wanaye walinichukia kutokana na kujipendekeza kwa baba yao kama kwamba, mimi ndiye niliyekuwa mtoto wa familia.
Unajua tena mtu akitoka shamba, halafu kwenye ukoo duni, akija mjini na akafikia kwa ndugu mwenye uwezo, ni lazima ataonyesha makeke ya kila aina. Ndivyo ilivyokuwa kwangu.
Nikiwa katika nyendo zangu za kuwania mabinti, nilimpata binti mmoja ambaye alikuwa ni mtoto wa mfanyabishara maarufu hapa jijini na anayefahamika sana. Huyu msichana alikuwa amemaliza masomo ya kidato cha sita na alikuwa akisubiri kwenda Chuo Kikuu cha Dar pale Mlimani.
Nilipokutana naye, nilimuingia kwa gea kwamba, nimemaliza kidato cha sita na natarajia kwenda kusoma nchini Marekani. Kwa kuwa nilikuwa nasoma masomo ya Kiingereza ya jioni, sikukosa vijineno vya kishikaji vya kimombo.
Siku moja niliamua kumpeleka yule binti nyumbani kwa mjomba na kumtambulisha. Wakati wa utambulisho nilisema mjomba ni baba. Mjomba hakujali kwani aliichukulia hiyo kamam heshima kw akule kunitafutia kibarua. Huyu binti aliamini kwamba mimi ni mtoto wa mtu ambaye kidogo ana nafasi.
Baada ya utambulisho huo, mjomba alitoka na mara Watoto wawili wa mjomba, mmoja wa kike na mwingine wa kiume waliingia.
Walipoingia, kabla sijawatambulisha, yule binti wa kike wa mjomba alimchangamkia huyu binti niliyekuja naye. Walikuwa wanajuana. ‘Kumbe hapa ndiyo kwenu.’ Alisema yule binti niliyemleta kwa mjomba. Mtoto wa mjomba akamjibu. ‘Ndiyo.’
Yule binti akasema, ‘ kumbe na (alinitaja jina) ni kaka yako, afadhali. Utakuwa wifi yangu… Yule mtoto wa mjomba alicheka kwa sauti. ‘Mwenzangu mtawezana na binamu yangu kweli! Kwanza ametoka shamba, halafu shule hamna, sijui lakini…..’
Nilimfuata binamu yang una kumsukuma. ‘unasema vitu gani wewe…’ nilimkabili binti wa mjomba kumnyamazisha asiendelee kuongea. Wakati huo huo mke wa mjomba ambaye alikuwa nje ya nyumba aliingia na kukuta ile vurugu. ‘Nini tena nyie, hata Mbele ya mgeni mnagombana, mnakuwa kama Watoto….’
Yule binamu yangu akasema, ‘Nashangaa, mimi nimemwambia Rafiki yangu kwamba binamu yangu (akataja jina langu) hajasoma, hawatawezana na kwamba, ametoka shamba juzijuzi. Ati Binamu amekasirika.
Yule binti mpenzi wangu aliingilia. ‘Kwani ni binamu yako au kaka yako. Hakusoma una maana gani? Kaniambia anakwenda chuo kikuu kimoja cha nchini Marekani mwaka huu…’
Kilifuata kicheko kutoka kwa mke wa mjomba na yule binamu wangu wa kike na wakiume na mtumishi wa Ndani.
‘Marekani ya wapi, Simiyu? Mke wa mjomba alisema akiwa na maana kwetu Simiyu.
Ilibidi yule binti aujue ukweli. Kwa kweli sijaona mtu anayetazama kwa dharau kama yule binti. Alinitazama kuanzia juu hadi chini na kusonya. Halafu huyoooo, alitoka na kuondoka zake. Nilisimama huku wale binamu zangu na mke wa mjomba wakinicheka. Leo hii nina adabu san ana ninajikubali bila masharti
Leave a Reply