Saudi Arabia yatarajia kusitisha mapigano

Saudi Arabia yatarajia kusitisha mapigano

Saudi Arabia inasema inatarajia mazungumzo yaliyoanza mjini Jeddah siku ya Jumamosi kati ya makundi ya kijeshi ya Sudan yanayozozana yatafikia usitishaji wa kudumu wa mapigano nchini humo. huku umoja wa Mataifa umeonya kwa majenerali wa nchi hiyo hawako tayari kusitisha mapigano.

Katika uthibitisho wa kwanza kwamba mikutano hiyo imeanza, wizara ya mambo ya nje ya Saudia ilisema pande zote mbili zinatambua haja ya kupunguza mateso wanayokumbana nayo watu wa Sudan.

Pamoja na kusitisha mapigano, lengo lilikuwa kuhakikisha usambazaji wa vifaa vya msaada na kurejeshwa kwa huduma muhimu.

Hakujawa na maoni yoyote yaliyotolewa na jeshi la Sudan au wapinzani wake wa kijeshi kuhusu mazungumzo hayo. Huku mkutano wa Jeddah ukiwa ni wa kwanza tangu mapigano yazuke zaidi ya wiki tatu zilizopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post