Sahani ya mlo unaofaa

Sahani ya mlo unaofaa

Sahani ya mlo unaofaa ndio leo katika Diet tunakuletea hiyo sahani ambayo imebuniwa na wataalamu wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Afya ya Jamii, Harvard na kuhaririwa na wataalamu kutoka Harvard.

Sahani hiyo ni muongozo wa mlo kamili unaofaa kwa afya, ikiwa utatumia sahani ya mlo huo basi itakufanya kuwa na afya njema.

Ninachokushauri ukimaliza kusoma dondoo hii, bandika nakala kwenye fridge au kabati lako hapo ili ikukumbushe kuandaa mlo kamili wenye afya!

Kwanza unapaswa kutambua kuwa sehemu kubwa ya mlo wako katika sahani yako iwe mbogamboga na matunda.

Hakikisha unaweka aina mbalimbali zenye rangi tofauti. Viazi mbatata havihesabiwi kama mbogamboga katika Sahani ya mlo unaofaaa kwa sababu ya madhara yake kwenye kiwango cha sukari mwilini.

Tumia vyakula vya nafaka isiyokobolewa

Vyakula vinavyotokana na nafaka isiyokobolewa kama vile ulezi, mtama, mchele wa brown vinaathari kidogo katika kiwango cha sukari mwilini na utengenezaji wa insulin kuliko vyakula vinavyotokana na nafaka iliyokobolewa.

Hivyo unashauriwa kuwa katika sahani yako ya mlo unaofaa, uwe na vyakula vya nafaka isiyokobolewa.

Nguvu itokanayo na protein

Samaki, kuku, maharagwe na njugu, vyote ni vyakula vinavyoleta afya kutokana na protein, vinaweza kuchanganywa na kachumbari.

Kwenye Sahani ya mlo unaofaa, vinafaa kuchanganywa na mbogamboga. Punguza matumizi ya nyama nyekundu and epuka nyama za kusindikwa kama bacon na sausage.

Mafuta yatokanayo na mimea kwa kiasi

Chagua mafuta yanayofaa ambayo yanatokana na mimea kama vile mizeituni, soya, mahindi, alizeti, karanga na mengineyo na epuka kutumia mafuta ambayo yameganda.

Kumbuka kuwa alama ya “low-fat” kwenye makopo ya mafuta haimaanishi “mafuta yafaayo kwa afya”.

Sahani ya mlo unaofaa inasisitiza utumiaji wa mafuta ya kupikia yatokanayo na mimea na haijamuwekea mtu kiwango cha juu cha asilimia ya kalori kutoka kwenye mafuta yanayofaa.

Kunywa maji, kahawa au chai

Sasa ukishamaliza kula jamani hicho chakula chako, epuka vinywaji vyenye sukari, punguza matumizi ya maziwa na vyakula vitokanavyo na maziwa mpaka mara moja au mbili kwa siku.

Punguza pia matumizi ya juisi mpaka glass ndogo moja kwa siku na hakikisha unakunywa maji kwa wingi, kahawa au chai.

Sahani ya mlo unaofaa pia inashauri watumiaji kuepuka vinywaji hivyo vyenye sukari, ambavyo ni chanzo kikubwa cha kalori kwenye mwili, wakati vikiwa na faida ndogo kiafya. 

Shughulisha mwili

Sahani ya mlo unaofaa pia inakumbusha kuweka mwili katika hali ya mazoezi kwani ni muhimu pia katika kupunguza uzito.

Ujumbe muhimu wa sahani ya mlo unaofaa ni kusisitiza kuhusu aina ya mlo unaofaa.

Aina ya wanga kwenye mlo ni muhimu zaidi kuliko kiwango cha wanga kwenye mlo, kwa sababu baadhi ya vyakula vya wanga mfano mbogamboga, matunda, nafaka zisizokobolewa na maharagwe vina manufaa kiafya kuliko zingine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post