Mastaa wa bongo waiteka youtube Kenya

Mastaa wa bongo waiteka youtube Kenya

Baadhi ya wanamuziki wa Bongo Fleva nchini wametajwa kuongoza orodha ya wasanii wanaotazamwa zaidi kupitia mtandao wa Youtube nchini Kenya.

Kupitia blogu ya ‘Nairobi Gossip Club’ imeshare orodha ya wasanii wanaotazamwa zaidi katika mtandao huo nchini Kenya huku orodha hiyo ikiongozwa na Diamond, Rayvanny, Harmonize, Zuchu, Israel Mbonyi na wengineo.

Hata hivyo kwa upande wa video ambazo zimetizamwa zaidi nchini humo anayeongoza ni mwanamuziki wa nyimbo za injili Israel Mbonyi kupitia wimbo wake wa ‘Nina Siri’ akifuatiwa na Jux kufuatia na wimbo aliomshirikisha Diamond wa ‘Enjoy’.



Kutokana na orodha hiyo katika upande wa ‘komenti’ baadhi ya mashabiki wa Kenya wameonesha kukerwa na orodha hiyo huku baadhi yao wakiwataka Wakenya kuacha kuwasapot wasanii wa nje na waanze kupenda vya kwao.

Wasanii wengine kutoka Bongo ambao wametajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Alikiba, Mbosso, Jay Melody, Jux, Marioo, Nandy na Phina.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags