Wakili wa Serikali afichua mawasiliano ya Diddy na wanaomtuhumu

Wakili wa Serikali afichua mawasiliano ya Diddy na wanaomtuhumu

Ni siku nyingine tena madhila yakiwa yanaendelea kumuandama nguli wa muziki wa Hip-Hop duniani Sean ‘ Diddy’ Combs, ambapo upande wa mashtaka jana Septemba 19 umefichua ushahidi kuhusu nguli huyo.

Mwanasheria msaidizi wa serikali anayeshughulikia kesi dhidi ya Diddy, Emily Johnson, ametoa taarifa mpya kufuatia kukamatwa kwa bilionea huyo Jumatatu Septemba 16, akieleza kuwa siku ambayo Diddy alinaswa kwenye video akimshambulia aliyekuwa mpenzi wake Cassie, kwenye ukumbi wa hoteli kulikuwa na mfanyabiashara wa ngono kabla ya shambulio hilo.

Mbali na hilo Johnson alifichua ujumbe wa maandishi kati ya Diddy na baadhi ya wanaodaiwa kuwa waathirika wa matendo ya mtuhumiwa huyo ambao majina yao hayakutajwa hadharani, huku muktadha wa mazungumzo yao ukiachwa bila kufafanuliwa.

Ujumbe mwingine ulikuwa na maelezo ya moja kwa moja. Mmoja wa waathiriwa alieleza kuwa Diddy alimpa michubuko ya kuvuja damu, wakati mwingine akidai kuwa alimpiga kichwani mara mbili kwa nguvu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags