Baada ya kuwepo kwa minong’ono kuhusiana na ‘rapa’ Lil Wayne kutochaguliwa kutumbuiza kwenye ‘Super Bowl Halftime’ mwakani mtayarishaji wa onesho hilo Jesse Collins amefunguka sababu za Wayne kuwekwa kando
Collins akiwa kwenye mahojiano na jarida la Variety amesema kila mwaka kunakuwa na Kamari ya kumchagua wa kutumbuiza kwenye tamasha hilo.
“Tunampenda Wayne, mashabiki wanatakiwa kujua kuwa kila mara kunakuwa na Kamari kuhusu nani atachaguliwa kufanya onesho hilo, lakini tutakuwa na onesho la kushangaza sana kutoka kwa Lamar na nadhani kila mtu atapenda, najua Kendrick atafanya kazi kwa bidii sana na kutoa onesho la ajabu,” Amesema Collins
Hata hivyo mtayarishaji huyo ameweka wazi kuwa anayechagua wasanii kutumbuiza kwenye tamasha hilo kila mwaka ni Jay-Z.
“Ni uamuzi ambao Jay anafanya, tangu tulipoanza kushirikiana na kipindi hicho, yeye amekuwa akifanya maamuzi kila mwaka, na yamekuwa ya ajabu, kila mara amechagua vizuri,” amemalizia Collins
Tangu 2021, Collins amekuwa mtayarishaji mkuu wa kipindi cha mapumziko cha Super Bowl, akishirikiana na Jay-Z na timu yake ya Roc Nation kuunda na kuwaanda wasanii watakao tumbuiza.
Utakumbuka wiki iliopita baadhi ya wadau na mashabiki walilalamika kuhusu Lamar kuchaguliwa kutumbuzia kwenye onesho hilo huku wakiamini kuwa aliyetakiwa kupewa jukumu hilo ni Wayne kwani Super Bowl itafanyika katika jiji alilozaliwa la New Orleans.
Leave a Reply