Wasanii hawa wanawafuasi na siyo mashabiki

Wasanii hawa wanawafuasi na siyo mashabiki

Na Masoud Shafii

Muziki kama tasnia nyingine umekuwa na mashabiki na wafuasi kwa wasanii, kwa mujibu wa wasanii wenyewe wamekuwa wakitoa maana ya maneno hayo mawili kwa kulinganisha watu wanaowafuatilia

Shabiki ni yule mtu anayemfuatilia msanii kipindi ambacho anatamba zaidi, mfuasi ni mtu ambaye atakuwa bega kwa bega kwenye kila kipindi ambacho msanii anapitia na huonesha kuendelea kumfuatilia bila kupunguza mapenzi ya kazi zake

Hawa ni baadhi ya wasanii wa muziki nchini ambao jicho la Mwananchi linawatazama kama wenye wafuasi, ambao wapo nao bega kwa bega bila kupunguza mapenzi

Ali Swalehe Kiba 'Alikiba' msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, kuna shabiki aliwahi kusema hajui kwanini anampenda msanii huyo. Licha ya muziki kupimwa kwa sauti nzuri na mashairi ya kupendeza shabiki huyo aliona kama hizo sio hoja kwake lakini yeye anabakia kumuelewa Alikiba kama Alikiba.

Mwaka 2010 mpaka 2014 Alikiba alikaa kimya kimuziki mpaka pale aliporudi na Mwana mwaka 2014, hiyo haikufanya mashabiki wake kumpotezea waliendelea kumfatilia kupitia mitandao ya kijamii na wengi wao wakionesha kutamani staa huyo kurudi kwenye game na kukimbiza kama kawaida na usisahau miaka hiyo ndio wasanii kama Diamond na wengine walikuwa wanakua kwa kasi.

Licha ya Alikiba kuonekana akifanya muziki kwa kuridhika na baadhi ya mashabiki wakiona kama kuna nafasi anazichezea kwa ajili ya yeye kufika mbali, bado wafuasi wake wakuwa na yeye bega kwa bega

Youngkiller Msodoki, ni msanii wa hiphop nchini ambaye mashabiki wake wamekuwa waaminifu kiasi huwezi kuta hata comment inayomponda msanii huyu kwenye mitandao ya kijamii, wengi wanamkubali kutokana na uwezo wake wa kufanya muziki na kujiweka mbali na skendo chafu pamoja na kiki.

Licha ya Youngkiller kutokuwa karibu na vyombo vya habari hiyo haijawazuia mashabiki kuendelea kumfatilia mkali huyo.

Youngkiller ambaye alipokelewa vizuri kwenye muziki wa rap kuanzia miaka ya 2010 na kuachia wimbo wa 'Dear Gambe' aliomshirikisha Belle 9 ameendelea kuwa rapa bora mpaka sasa hata akikaa muda mrefu bila kuachia wimbo anaporudi kuachia wimbo mashabiki wamekuwa wakimpokea.

Roma Mkatoliki huyu ni msanii wa hip hop nchini Tanzania ambaye amejizole umaarufu kutokana na nyimbo zake za kiharakati na zenye kugusa jamii moja kwa moja. Roma mkatoliki ni miongoni mwa wasanii ambao wanawafuasi na sio mashabiki

Roma anaushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia nyimbo zake zinaweza teka hisia za wasikilizaji kwa namna moja au nyingine, Aprili 2017 Roma, Moni Centrozone na mtayarishaji wa muziki Binladen walipotea katika mazingira ya kutatanisha, nguvu ya mashabiki ilionekana na baadhi ya wadau mbalimbali walipaza sauti kutaka kujua Roma alipo mpaka pale alipopatikana.

"Nimechapwa mijeredi nimevunjwa bila huruma siku tatu nimefumbwa macho mikono imefungwa nyuma asante mliopaza sauti nimeiona nguvu ya umma" aliimba Roma kupitia wimbo wake wa Zimbabwe

Roma alianzisha mchakato wa kumchingia msanii mwenzake Ney Wa Mitego baada ya kuitwa na BASATA kufuatia kutoa wimbo wake wa 'Nitasema' ukidaiwa kuwa na makosa

Roma Mkatoliki kwa sasa yupo nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 4, licha ya kutokuwa karibu na media za Tanzania bado amekua akipata sapoti na kukutana na mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii

Hao ni baadhi ya wasanii wenye wafuasi maoni yako ni yapi msanii gani unaona anawafuasi na sio mashabiki?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags