Tems msanii wa kike afrika aliyeteuliwa vipengele vingi Grammy

Tems msanii wa kike afrika aliyeteuliwa vipengele vingi Grammy

Mwanamuziki kutoka Nigeria Tems ameendelea kufanya vizuri katika tasnia ya burudani ambapo ametajwa kuwa msanii wa kwanza wa kike kutoka Afrika kutajwa kwenye vipengele vingi katika tuzo za muziki za Grammy.

Tems ametajwa kuwania tuzo katika vipengele kama Best African Music Performance, Best Global Album, na Best RnB Song huku album yake ya ‘Born In The Wild' ikiendelea kumpatia mafanikio.

Tems anakuwa msanii wa kike wa kwanza Afrika kuteuliwa katika kategori za Kimataifa ambapo wimbo wake wa ‘Burning’ ukiingia katika kategori ya RnB, hatua hii inamfanya Tems kuwa msanii wa kwanza kutajwa katika tuzo za Grammy mara sita.

Utakumbuka usiku wa kuamkia leo Novemba 9, Grammy waliachia listi ya majina na vipengele vya tuzo hizo huku mwanadada Beyonce akiongoza kwa kutajwa kwenye vipengele 11.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags