Diddy aomba dhamana kwa mara nyingine

Diddy aomba dhamana kwa mara nyingine

Baada ya kugonga mwamba kwa mara kadhaa kuhusiana na kuomba dhamana ya kuachiwa huru huku akisubiria kesi yake ianze kusikilizwa mahakamani, mkali wa Hip hop Marekani Diddy Combs amewasilisha tena ombi la dhamana kwa jaji anayesimamia kesi yake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tmz, wanasheria wa Diddy mapema jana Ijumaa Novemba 8, 2024 waliwasilisha ombi la dhamana huku wakiwa na pesa tasmilim dola milioni 50 pamoja na kukubaliana na masharti ya kutosafiri kwenda nchi nyingine wala kutishia mashahidi ili mkali huyo aweze kuachiwa huru.

Hoja hiyo inafanana na ile ambayo waliwasilisha mwenzi Septemba na kukataliwa sasa wanasheria hao wamerudi tena huku wakitilia mkazo suala la Diddy kuachiwa kwa sasa kwani wapo baadhi ya watu walituhumiwa kwa kesi kama hizo na walipewa dhamana.

Kwa sasa Diddy amezuiliwa katika jela ya MDC Brooklyn baada ya kukataliwa dhamana kwa zaidi ya mara mbili huku jaji anayendesha kesi yake akidai kuwa Combs hawezi kuachiwa huru kwani serikali inaamini mshatakiwa ni hatari kwa jamii.

Ikumbukwe Diddy alikamatwa na kutupwa gerezani Septemba 16 jijini Ney York kwa makosa makubwa ya unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Me 5, 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags