Rock D: Askari magereza aliyeibukia katika muziki

Rock D: Askari magereza aliyeibukia katika muziki

Niajeee! Wanangu wa Mwananchiscoop najua mtakuwa mmetumisi sana, basi leo tumekuja kukata kiu yenu na shauku mliokuwa mnaisubiri kuhusu new mwananchiscoop na leo kwenye burudani nimekisogezea mwanamuziki chipukizi kutoka katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam ambapo safari yake ya muziki ilianza rasmi mkoani Iringa mwaka 2014

Abdallah Deodafus Rangimoto also known as ROCK D is an Tanzanian musician na nje ya kufanya muziki yeye ni  askari magereza, alipata umaarufu baada ya kutoa ngoma yake ambayo ilifanya vizuri ya “Tawile” nyimbo iliemleta rasmi mjini na kifanya ikapendwa na watu wa kila rika. Kwasasa yuko jikoni anapika video ya nyimbo ambayo ishatoka inayojulikana kwa jina la “  Sijiwezi”

Rock D pia ni mwanamuziki wa live band ya magereza ambayo inafahamika kwa jina la “Mkote Ngoma” ilioko jijini Dar es Salaam katika gereza la Ukonga, na vitu ambayo hupendelea kuvifanya zaidi ni kuimba, kuskiliza muziki na kucheza mpira wa football.

Kupitia mwananchi scoop Rock D alifungunga na kueleza kuhusu changamoto anazo zipitia kwasasa.

 “Changamoto kwasasa katika mziki wangu ni kumpata meneja ambaye atakae weza kusimamia mziki wangu, ili niweze kufika mbali na matamanio yangu yaweze kutimia ya kuwa mwanamuziki mkubwa kama walio fanikiwa katika nchi yetu na dunia Kwa ujumla” Amesema Abdallah Rangimoto

Historia ya Abdallah kwa ufupi

Amezaliwa mkoani Kilimanjaro ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watano, elimu ya msingi aliipata katika shule ya msingi Ukonga jijini Dar es salaam na mwaka 2007-2010 secondary shule ya Korongoni.

Rasmi aliajiriwa na magereza mwaka 2012 pia alifanikiwa kupata cheti cha muziki kutoka katika chuo cha TCTA ambapo alipojifunzia rasmi kuhusu masuala ya muziki.

Aidha alimalizia kwa kueleza kuwa “Kwa sasa nawaomba mashabiki wangu wakae mkao wakula wa video yangu mpya ya nyimbo yangu ya sijiwezi Kwa kuweza kuitizama na waweze kusubscribe you tube channel yangu ya “ROCK D Tz” bila kusahau kunifollow Instagram yangu rocks_tz.

We love ROCK D because he is a young man and he does well through his music he knows how to miss it and give the community something they love, so we advise budding musicians to follow in   Abdallah footsteps in order to be musically successful

 






Comments 14


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post