Nigeria yaruhusu utumiaji wa noti za zamani

Nigeria yaruhusu utumiaji wa noti za zamani

Benki Kuu nchini Nigeria (CBN) imetoa ruhusa ya utumiaji wa note za zamani na kueleza kuwa pesa hizo zitasalia kuwa pesa halali hadi mwisho wa mwaka kulingana na uamuzi uliotolewa na mahakama kuu mapema mwezi huu. 

Benki nyinginezo pia zimeagizwa kutii uamuzi wa mahakama ulioruhusu noti za zamani na mpya za naira kutumiwa kwa wakati mmoja hadi tarehe 31 Desemba.

Ukosefu wa noti mpya zilizoundwa na naira ulisababisha uhaba wa pesa katika nchi ambayo 40% ya watu hawana akaunti za benki.

Ikumbukwe tu Oktoba iliyopita, benki kuu ilibuni upya noti za juu zaidi ili kukabiliana na ughushi, uhifadhi wa fedha na ukosefu wa usalama unaochochewa na utekaji nyara kwa ajili ya fidia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post