Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ari Nagel kutoka Brooklyn nchini Marekani kwenye siku ya baba duniani inayoadhimishwa kila mwaka Juni 16, amesheherekea siku hiyo kwa kupata mtoto wake wa 165 huku wanawake wengine 10 waliopo Marekani, Canada, Afrika, Asia na Ulaya wakiwa na mimba zake kwasasa.
Ari ambaye ni profesa wa hisabati mwenye umri wa miaka 48, amemkaribisha mtoto wake wa 165 kutokana na juhudi zake za kutoa mbegu za kiume ‘Sperminator’ kwa kusaidia wanawake wanaotaka kuitwa mama.
Licha ya kuwa na watoto wengi mwanaume huyo amedai kuwa huwa hakutani na wanawake hao kimwili bali hutoa mbegu zake kupitia Clinic maalumu nchini humo hii ni baada ya kukutwa na magonjwa ya kurithi.
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa mpaka kufikia sasa mwanamume huyo bado hajaonana na kabisa na watoto wake 34 huku wengine akionana nao kipindi cha likizo.
Agost mwaka huu atatimiza miaka 49 na amesema akitimiza miaka 50 ndio ataacha kugawa mbegu zake, kwani hataki watoto wanaozaliwa wawe na changamoto yoyote ya kiafya.
Mwanaume huyo amedai kuwa yupo tayari kutoa msaada kwa mama zao kwa kadiri ya uwezo wake, lakini amesema asilimia kubwa ya wanawake anaowapa msaada wa mbegu zake hawataki kumpa majukumu ya kuhudumia watoto bali wanalea wenyewe.
Hivyo Profesa huyo ameleeza namna ambavyo akumbuka watoto hao kwa kudai kuwa ameweka picha za watoto wote ofisini kwake, tarehe zao za kuzaliwa pamoja na anuani ili kurahishisha mawasiliano na mama zao.
Ari Nagel kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni ameeleza hali yake ya mahusiano kwasasa na kudai kuwa ni ngumu kwake kupata mpenzi kwa sababu wanawake wengi wanamkataa pindi wakijua ana watoto wengi na ni masikini.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply