Anaconda: nyoka hatari asiyeua kwa sumu

Anaconda: nyoka hatari asiyeua kwa sumu

Katika listi ya nyoka hatari zaidi duniani uwezi ukasahau kumtaja Anaconda ambaye hufahamika kama Green anaconda au Giant anaconda.

Filamu nyingi zimetolewa kuelezea hatari ya nyoka huyu lakini sifa za hatari yake ni zaidi ya ukubwa wake ambao huwatisha wengi.

Unaambiwa kuwa nyoka huyu hupatikana Marekani Kusini na cha kushangaza haui kwa sumu bali ana nguvu na misuli ya kipekee kumbana adui wake hadi kufa na kisha kumla mzima.

Kulingana na simulizi ya Makala maalum kumhusu nyoka huyo iliyochapishwa na BBC Earth, anaconda anaweza kuwa na urefu wa hadi futi 25 na uzito wa hadi kilo 136.

Nyoka huyu ndiye mzito zaidi wa aina yake na wakati mwingi anaishi maji au karibu na maji ambako anafanya mawindo yake.

Chakula na makazi

Nyoka wa anaconda hupenda kuishi karibu na maji na wana uwezo wa kusalia ndani ya maji hadi kwa dakika kumi kwa akati mmoja kwa sababu ya uwezo wa mapafu yao . Sifa hiyo huwawezesha kuwavizia wanyama wengine kimya kimya bila kugunduliwa.

Wanyama wengine wanaoishi karibu na maji au kuja kunywa maji ndio hutumiwa kama mlo na nyoka wa anaconda.

Iwapo kuna nyoka anayeweza kujificha kwa njia ya kistadi majini basi ni huyu. 

Anaconda wana uwezo wa kuficha miili yao majini na kuinua kichwa ili kuelea majini na kutumia hilo kama njia ya kuwanasa wanyama wengine

Ole wako iwapo hutagundua mapema kwani kitakachofuata ni mauti.

Aina ya anaconda wanaoishi Marekani Kusini huwa hawawindi bali wanyama wanaolengwa kama mlo hujipata katika maeneo yao na kushambuliwa.

Nyoka asiyeua kwa sumu

Nyoka huyu hana sumu kama nyoka wengine. Hatari ya watu kuogopa nyoka ni kuumwa na kuachiwa sumu hiyo mwilini, lakini anaconda hana uwezo wa kuua kwa sumu.

Uwezo wake wa kuua na nguvu za misuli yake ya mwili kuvunja na kumbana adui ili kuzuia kutembea kwa damu .Mgando wa damu hukosesha hewa kufika kwenye moyo ambao huacha kupiga.

Pindi anaconda anapogundua moyo umekoma kupiga basi kinachofuata ni kukumeza mzima kwani hana uwezo wa kuchana wanyaam wengine vipande vipande kabla ya kuwala kwa hivyo anategemea maumbile yake ya kinywa kinachoweza kupanuka kwa urahisi ili kumeza mlo wake kuanzia utosini hadi miguuni.

Utashangaa kumuna nyka huyu akiendelea kumupua licha ya kusakamwa na mnyama mkubwa katika kinywa chake.Anapumua vipi huku akiwa amezibwa na mnofu wa mnyama mzito au mkubwa zaidi?

 Anaconda ana kifaa maalum kama bomba dogo linalotoka kinywani mwake ambalo hutokea nje ili kuvuta pumzi.

Wakati anaendelea kumeza mlo wake bila kujali anatoshanaje,yeye huendelea kupumua kama kawaida na ndiop maumbile yanayomfanya kuwa hatari zaidi kwani ukubwa wa mnyama anayemwinda haumtishi kwani atammeza .

Meno yake pia yameelea kwa ndani ili kuyrahisisha kuteleza kwa mnyama yeytote anayefaulu kumvunja nguvu na kisha kuanza kummeza.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post