Mfahamu Bi Aziza mwanamke mwenye urafiki na nyoka

Mfahamu Bi Aziza mwanamke mwenye urafiki na nyoka

Nyoka huchukuliwa kuwa hatari kubwa, waerevu na mara nyingine hata kuhusishwa na imani potofu na uchawi katika baadhi ya jamii za Kiafrika.

Kwa kawaida nyoka anakuwa juu ya orodha ya mambo ambayo mtu anaogopa maishani mwake. Lakini hali ni tofauti kabisa kwa Aziza Swaleh mkazi wa Msambweni kusini mwa Pwani ya Kenya ambaye ameamua kufuga nyoka.

Kokosi cha BBC Swahili kilimtembelea Bi. Aziza ili kufahamu zaidi undani wa kazi hii adimu na ukaribu wake na baadhi ya nyoka wanaoaminika kuwa wakali na wenye sumu.

Kwa  mfano nyoka aina ya chatu wakubwa na wazito kweli kweli , pilka pilka za kuwalisha mamba na wanyama wengine wa ajabu.

Lakini kwake yeye haya ni mambo ambayo hayafai kuwapatia wasiwasi watu kwani ni njia mmoja ambayo jamii yake inapata kipato cha kila siku.

''Nilipokutana na mpenzi wangu miaka kadhaa iliyopita na ambaye ni mume wangu sasa na baba ya wana wangu, nilipiga moyo konde na kuamua kujifahamisha kuishi katika mazingira moja na wanyama ambao yalikuwa wakifugwa na mume wangu hata kabla ya kufunga ndoa'' anasema Aziza.

Kazi ya kuwafuga  wanyama pori

Aziza na mume wake ambaye anayefahamika kama Arafat Manyoka ndio wanaoendesha bustani la Jungle snake park lililopo Kaunti ya Kwale nchini Kenya.

Bustani hili ni maarufu katika eneo hili kwa kuwafuga wanyama mbalimbali.

Kwa hiyo kazi nyingi za kuwatunza wanyama hawa zimo mikononi mwa Aziza na mume wake.

Mwanadada huyu anawashangaza wengi kila kwa kuwa mmoja wa wanawake ambao wana ujasiri wa kutosha kuwa na uhusiano wa karibu wanyama wanaoogopwa hasusan na jinsia ya kike.

Lakini kwa Aziza uhusiano wake na wanyama hawa kwa mfano mamba, nyoka wa aina moja na wanyama wengine ambao wanapoonekana wanaibua imani na dhana tofauti miongoni mwa jamii za Afrika na pia uoga unaoandamana na kuwatizama tu hata kwa mbali  Ila kwake mwanadada huyu  hatishwi wala kubabaika akiwa miongoni mwao.

''Kazi zangu za karibia kila siku ni kuhakikisha kwamba ninawaangalia wanyama waliokwenye bustani letu, hasa mimi hufurahia sana kuingia kwenye sehmeu waliopoa nyoka waliowakubwa kwelikweli, nina majukumu ya kuhakikisha kwamba eneo wanaloishi ni safi kwa hio hulifagia na pia kuhakikisha wana maji ya kutosha, Joka kwa jina Melita ni rafiki wangu sana ”anasema Aziza.

Aziza Swaleh ameishi hapa kwa zaidi ya miaka mitano , na anasema kwamba kidiri anapoendelea kuwahudumia wanyama hawa ameendelea kuwa na ujasiri na pia kuelewa vyema wanyama wanaofuga.

Mwanadada huyu ambaye ni mama pia anayachukulia majukumu ya kulinda bustani hili jinsi kila mtu hutunza riziki yake kwa udi na uvumba na kwa heshima kuu ikizingatiwa kuwa yeye miongoni mwa wanawake wachache ambao hujumuika na wanyama hawa.

Katika Bustani la Jungle kando na nyoka kuna wanyama wengine kama vile mamba, kobe, mburukenge, na bundi miongoni mwa wengine.

Wanyama hawa wote huhitaji kula wengine kila siku na wengine hula baada ya wiki kadhaa. Aziza anajua kila hitaji la mnyama kwa wakati wake.

Makaazi yao yako ndani ya bustani lenye wanyama hawa ila Wanyama wenyewe wako katika mazingira ya kufungwa kisawasawa.

Bustani hili la jungle linakuwa ni eneo ambalo watu hutoka mbali kujionea Wanyama mbalimbali.

Aziza ni miongoni mwa wafanyikazi hapa ambao pia anatoa onyesho kwa kuwadekeza na kuwabeba Wanyama hawa iliwageni wawe na picha ya urafiki wake na Wanyama hao

“Ndio kunao wengi ambao hunishangaa sana , na hata majirani wanakuwa wananishangaa ni vipi tunaishi sehemu mmoja na Wanyama ambao wanaitikadi na dhana tofauti miongoni mwa jamii hasa bara Afrika.

Kwa kuwa ni na wanangu wadogo nimechukua fursa ya kuwafunza kuhusiana na ulimwengu wa wanyama hawa ”anasema Aziza.

Bustani hili la Jungle linatoa maonyesho kwa wageni mbalimbali ambao huingia hapa aidha kama watalii wa ndani au wa nje kujipumbaza kwa kuona hawa  maonyesho yasioyakawaida hutolewa kwa mfano wakiwalisha nyoka hao au hata mamba,

pia wanafunzi kutoka shule mbalimbali  hutembea hapa kusoma kuhusu maisha ya baadhi ya Wanyama  na kwa hio Aziza ambaye ni mke wa mwenye bustani hili alianza kupendezwa na kazi ya mume wake na hakuwa na budi kujifunza ulimwengu huu ambao ni tofauti na malezi yake

''Kwa wakati huu siogopi mnyama wowote ndio watu wanadhana tofauti kuhusu kukaa karibi na mnyama kwa mfano bundi ila hizo ni itikadi tu kwangu mimi nimewazoea kabisa na sioni nikiishi mbali na Wanyama hawa ”anasema Aziza.

Historia yake ya kuumwa na Nyoka

Japo Aziza ni mzaliwa wa Kwale anasema kwamba uhusiano wake na wanyama kama nyoka haukuwa mzuri wakati alipokuwa mdogo alijipata katika ajali alipong’atwa na nyoka mguuni.

Ni kisa ambacho hajakisahau kwani nusura apoteze mguu wake ila alipona baada ya matibabu.

''Nilikuwa binti wa miaka 16 na tulikuwa na wasichana wenzangu tukitoka dukani mara niliumwa na nyoka mguuni na hata sasa nina alama ya tukio hilo. Kutoka wakati huo niliwaogopa sana na sikutaka kabisa kukaribia sehemu walioko, lakini amini usiamini sasa mambo ni tofauti na nimejenga urafiki wa kipekee na nyoka tunaowafuga hapa,''Aziza anasema.

Wakati anazungumza kuhusu kazi yake ya kuwatunza wanyama hawa yeye anasema kwamba anafahari kwamba kama mwanamke amechukua mkondo tofauti na kazi zinazofanywa na wanawake ila hajutii na kila siku inakuwa ni wakat iwa kusoma na kutangamana na wanyama walioko katika bustani lao

 Na kwa hio kila kuchao baada ya shughuli zake za kuwa mke na mama kwa watoto wake utampata akiwa na shughuli kemkem za kuwalisha wanyama hawa minofu ya nyama imemwagwa sakafuni huku ukimona Aziza akiwachagulia wanyama kulingana na mahitaji yao , Kwa mfano anasema kwamba Nyoka wanakula kila baada ya wiki mbili au tatu , na sana sana wanawalisha Panya au sungura ambao wanafugwa kama chakula chao , Upande mwengine anawalisha mamba , mamba wanakula minofu ya nyama ambayo wananunua madukani na kisha kuwapasua kwa vipande vipande na kuwatupia katika sehemu spesheli walipofungiwa .

Lakini swali kubwa tulilokuwa tukijiuliza wakati tukiwa kwenye bustani hili la Jungle ni vipi anamudu kuwashika Wanyama hawa bila kushikwa na uoga …na je hana wasiwasi kwamba wanayama wanaweza kumgeukia alijibu kwa ujasiri

Jibu lake ni kwamba yeye ni mke wam moja ya watu wanaojulikana kupambana na wanyama kama hao na kwa hio anajitambua kama Jike simba kwa ukakamavu wake

Yote tisa kumi ni kuwa anasema cha muhimu katika kuwahudumia wanyama hawa ni kuhakikisha kwamba wanapewa chakula kwa muda unaotakikana na pia kupumzika vya kutosha

Kwa mujibu wa Aziza mnyama yeyote hutambua yuko hatarini wakati mazingira aliyepo yanapobadilika ghafla au anapokosa chakula au maji naye hana budi kutupa makucha yake kujilinda.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post