Changamoto zinazowakumba madereva wa maroli  barabarani

Changamoto zinazowakumba madereva wa maroli barabarani

Waswahili wanasema kazi ni kazi ilimradi mkono uende kinywani, lakini ndani ya kazi hizo ambazo watu wanazifanya yapo mengi wanayokumbana nayo yanayowafikirisha kiasi cha kuacha kazi, lakini kwao siyo rahisi kihivyo kutokana na familia kuwategemea.

Moja ya kazi ambayo vijana wengi wamekuwa wakivutiwa nayo kuifanya kwa siku za hivi karibuni na kusafirisha mizigo kupeleka katika nchi nyingine, yaani kazi ya uendeshaji maroli ya mizigo, hii ni kutokana na wengi wao kutokupenda kazi za kuhangaika.

Japo kazi hii inawapatia maokoto ya kutosha lakini kwa maelezo yao ni kazi ambayo wanakutana na changamoto nyingi wawapo barabarani, kutokana na hilo Mwananchi Scoop imekutana na dereva ambaye anafanya safari kutoka Dar es Salaam kwenda Congo Hassan Juma Mkwanda maarufu Big Fish ambaye ameelezea changamoto zinazowakabiri katika kazi hiyo.

Hassan ni muhitimu wa Diploma in Journalism kutoka katika chuo cha DSJ (2020) baada ya kukosa ajira sehemu mbalimbali alizokwenda kuomba aliamua kuchukua jukumu la kwenda kujifunza udereva ili asiweze kubaki nyumbani wakati akisubiria ajira, Big Fish amefunguka kuhusiana na kazi yake hiyo.

“Changamoto zipo nyingi lakini changamoto kubwa ambazo zinapelekea tukate tamaa ya kwanza ni ubovu wa barabara na hii ndiyo linapelekea kutokea kwa ajali kila siku” amesema Big Fish

Aidha wakati wa mahojiano hayo pia dereva huyo alifunguka machache kuhusiana na madereva malori wengi kuwa na desturi ya kununua wadada wa bei rahisi nyakati za usiku barabarani ambapo aliweka wazi kuwa

“Watu wengi wanadhani kuwa ni utani lakini suala hilo lipo kabisa, na madereva wengi wananunua wanawake japo siyo wote kutokana na kila mtu na haiba yake, wapo baadhi ya madereva wao husafiri tu kwa sababu ya mambo kama hayo, lakini sisi wengine tunajitambua, ukiwa umeacha familia nyumbani huwezi kufanya mambo kama hayo” amesema Big

Hata hivyo Big Fish amemalizia kwa kuiomba Serikali kuwatazamia madereva kwa jicho la tatu kutokana na changamoto wanazokumbana nazo, ambapo alieleza kuwa anaamini Serikali haishindwi na jambo ikiamua kuwasaidia matatizo kama hayo haichukui hata muda mrefu kutatuliwa.

Pia Hassan aliwashauri vijana kuacha kubweteka na kusubiri ajira kwani siku hizi kupata ajira ni ngumu huku akiwataka kutafuta ujuzi ambao unaweza kumuingizia kipato.

Mwananchi Scoop pia tukafanya mazungumzo na dereva mwingine ambaye anafanya safari zake kutoka Tanzania kwenda Burundi Abdully Wakili ameleeza changamoto wanazokumbana nazo baadhi ya madereva.

“Changamoto kubwa tunayokumbana nayo tukiwa barabarani ni kufanyiwa vurugu tunapokuwa kwenye nchi za watu, wanatuvunjia vioo, wanatuibia mafuta, halafu tukirudi nyumbani mabosi wanatuona sisi kama wezi, hii ndiyo changamoto kubwa ambayo inapelekea baadhi yetu kuacha kazi” amesema Abdully

Aidha dereva huyo alitilia mkazo suala la trafiki kusumbua madereva barabarani huku akiiomba Serikali kulifanyia kazi suala hilo kwani wamekuwa wakipoteza pesa nyingi kutokana na kupigwa faini mara kwa mara






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post