Mbunge wa zamani wa Afghanistan auawa nyumbani kwake

Mbunge wa zamani wa Afghanistan auawa nyumbani kwake

Mbunge wa zamani wa Afghanistan Mursal Nabizada mwenye umri wa miaka 32 na mlinzi wake wameuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake katika mji mkuu Kabul.

Kaka yake na mlinzi wa pili walijeruhiwa katika shambulio hilo siku ya Jumapili.

Mursal alikuwa mmoja wa wabunge wachache wa kike waliobaki Kabul baada ya Taliban kunyakua mamlaka mnamo Agosti 2021.

Tangu Taliban warudi madarakani mwaka 2021, wanawake wameondolewa katika karibu maeneo yote ya maisha ya umma. Msemaji wa polisi wa Kabul Khalid Zadran amesema kuwa vikosi vya usalama vimeanza uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.

Mbunge wa zamani Mariam Solaimankhil alisema Bi Nabizada alikuwa "mfuatiliaji wa kweli, mwanamke mwenye nguvu, mzungumzaji ambaye alisimamia kile anachoamini, hata katika hali ya hatari."

"Licha ya kupewa nafasi ya kuondoka Afghanistan, alichagua kubaki na kupigania watu wake," aliandika kwenye Twitter.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post