Mambo ya kuzingatia unapotaka kuweka dreadlocks

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuweka dreadlocks

Hellow!! vipenzi vyangu kama kawaida yangu lazima tukutane kwenye segment yetu pendwa ya Fashion ili kujuzana mambo mbalimbali kuhusu urembo na style tofauti tofauti za ndani na nje ya nchi, kwa mara nyengine nikukaribishe.

Leo katika Fashion tutazungumzia mambo muhimu ya kujua unapotaka kuwa na nywele za DreadLocks, endelea kuwa na mimi mwanzo mpaka mwisho utanishukuru baadaye.

Ukweli ni kwamba dreadlocks ni mtindo wa nywele ambao hauna kazi kubwa sana ukilinganisha na mitindo mingine, lakini ni muhimu sana kuziangalia na kuzijali maana unaweza kuziharibu kwa kutozitunza.

Kama unataka kuwa na dreadlocks, zingatia mambo haya ambayo unatakiwa kuyajua ndiyo maana nimekusogezea hapa katika ulimwengu wa Fashion.

Unachotakiwa kujua kwanza nywele huwa na asili tofauti, usijitese kwa kulinganisha ukuaji na ubora wa nywele zako na mtu mwengine, kuna wale ambao wana nywele nyingi, wengine nyepesi, wengine zinakua haraka, wengine zina rangi fulani nk.

Hata kama umeanza kutengeneza dreadlocks na rafiki yako, ukuaji huwa tofauti, ruhusu nywele zako kukua vile zinavyotaka na usijipe shida ya kulinganisha au kutamani zikue katika namna fulani. Maisha mafupi, acha nywele zako ziku-surprise na ridhika na ukuaji wake.

Kwenye jamii zetu kuna mitindo bado inaangaliwa kwa jicho la tofauti, dreadlocks zikiwemo. Unajua ukiwa na dreadlocks ukikatiza tu sehemu fulani wanaweza kudhani wewe ni mtu wa namna fulani yaani ni muhuni ila unatakiwa ujifunze kuwa  dreadlocks au mtindo mwingine wa nyweli unakufanya uwe mwenye kujiamini na kujikubali jinsi ulivyo na urembo  wako.

Pia hakikisha usichanganye mafuta unayotumia ya nywele hiyo itakufanya usione ukuaji halisi wa nywele zako na product inayokufaa kutumia kwa sababu ya kubadilisha vipako hivyo vya nywele.

Kutoruhusu mawazo ya mtu mwengine kwa sababu mwisho wa siku wewe ndiye mwenye maamuzi ya kuangalia kitu gani unapenda katika urembo huo.

Kama unataka kuanza, usiruhusu watu wanavyokufikiria ikusumbue kiasi kwamba hauanzi kwa sababu yao, kama unapenda na unauwezo wa kufanya basi fanya.

Dreadlocks zinavipindi tofauti katika ukuaji, jipende na uzipende wakati wote. Kuna kipindi kinaitwa ‘ugly stage’, hiki ni kile ambacho nywele ni ndogo sana na hata haziko muonekano ambao utapenda watu wakuone nazo, lakini bado katika hali hiyo jiangalie kwenye kioo na ujikubali, ujipende katika hali zote.

Kama mwanadada Rehema James anavyoelezea yeye alijikubali na kujipenda kutokana na muonekano wa nywele yake ya Dreadlocks “kujipenda na kujikubali ambako nimekupata kutokana na kuanza safari yangu ya dreadlocks kumenisaidia sana hata kujiamini, kuwa mvumilivu wakati zinakua, hivyo mtu unapaswa kujifunza kupenda na kujipenda katika kila hatua ya ukuaji wa hizo nywele”.

Kingine unachotakiwa kujua nywele zinaongezea utofauti na kujiamini kwako, usiogope kuwa na dreadlocks maana ni mtindo ambao kwa nywele za kiafrika unapendezea sana mwanamke huwa na muonekano mzuri lakini kwa wale wanaopenda mtindo huo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post