Mchezaji wa ‘klabu’ ya PSG Ashraf Hakimi ambaye yupo Tanzania kwa ajili ya mapumziko na kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii, kupitia taasisi yake ya ‘Achraf Hakimi Foundation’ ametoa msaada kwa wanafunzi wenye uhitaji mkoani Arusha.
Akiwa na mwenyeji wake Rais wa ‘klabu’ ya Yanga Eng. Hersi Said, Hakimi siku ya leo Juni 27 alitembelea katika shule ya watoto wenye uhitaji maalumu ya ‘Patandi Sekondari’ na kutoa misaada wa vifaa mbalimbali zikiwemo Kompyuta 50, mashine za kuchomea taka, vifaa vya nukta nundu, samani na vinginevyo.
Aidha wakati wa kukabidhi vifaa hivyo beki huyo alimshukuru Rais wa Yanga Eng. Hersi Said kwa kuwa mtu maalumu katika safari yake.
“Nimefurahi kuwa nanyi na kutumia sehemu yangu ya likizo hapa Tanzania. Niliongea na kaka yangu Hersi tulipokutana Paris na amekuwa sehemu muhimu ya Safari yangu ya kuja Tanzania. Kutoka moyoni napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wote wanaofanya kazi kubwa ya kuwalea watoto hawa na ninaamini siku moja nitakuja tena kuwa pamoja nanyi”
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa taasisi ya Hakimi kutoa msaada nje ya nchi yake ya Morocco.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply