Fahamu njia tano sahihi zitakazokuwezesha kupiga hatua kwenye kilimo

Fahamu njia tano sahihi zitakazokuwezesha kupiga hatua kwenye kilimo

Vijana wengi sana sasa wamehamia kwenye kilimo. Kama na wewe ni mmoja wapo, usidanganywe na wale watu wa matikiti 100 kwa milioni 100, UTAPIGWA BOSS!

Basi sasa, unafahamu njia zitakazokuwezesha kupiga hatua kwenye kilimo? Nakudondoshea njia chache na rahisi zitakazokuwezesha mkulima kufikia malengo yako kwenye sekta  ya kilimo.

.Fanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao au mazao

.Fanya kilimo cha umwagiliaji. 

.Tumia njia za kisasa za kilimo

.Tumia wataalamu wa kilimo kabla hujaanza kulima zao/mazao yako

kufanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao unalotaka  kulima  ,tumia wataalamu wa kilimo ambao wanaweza wakakushauri kulingana na eneo unalotaka kulima sio kila ardhi inakubali kulima zao fulani kunasehemu udongo wake hauna rutuba hata ukilima zao halioti.

Kilimo cha umwagiliaji, kufanya kilimo cha umwagiliaji ili uweze kuzalisha kipindi ambacho wengine  hawawezi kuzalisha kwa wakati huo ili uweze kuuza mazao yako kwa bei nzuri.

Tumia wataalamu wa kilimo, kufanya hivyo kutakusaidia kupata maelezo sahihi kutoka kwa wataalamu wa kilimo ili uweze kulima kulingana uhitaji wa soko la bidhaa.

Tumia njia za kisasa za kilimo kama vile trekta, kwa kutumia njia hizo zitakurahisishia kazi wakati wa kulima zao lako.

 Fuatilia tips hizi uweze kuwin kwenye sekta hii ya kilimo. Changamkia fursa kijana!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post