Fahamu kiundani kuhusu aleji (allergies)

Fahamu kiundani kuhusu aleji (allergies)

Mzio au aleji (allergy) ni matokeo ya mpambano uliopitiliza kati ya kinga ya mwili na kitu chochote (ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa mwili) inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili.

ALEJI HUSABABISHWA NA NINI?

Kwa kawaida kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu mbalimbali hatari kwa afya kama vile vimelea vya bakteria na virusi, lakini wakati mwingine inaweza kupambana pia na vitu ambavyo havina madhara yeyote kwa mwili (ambavyo huitwa allergens) na kutengeneza kemikali mbalimbali ikiwemo histamine ambayo hupambana na allergens hizo. Watu wenye aleji/mzio huwa na hisia zisizo za kawaida za mwili dhidi ya baadhi ya vitu.

Baadhi ya visababishi (allergens) ni pamoja na vumbi vumbi, baadhi ya dawa, baadhi ya vyakula, kung’atwa na wadudu kama vile nyuki, aina fulani ya uyoga, vumbi vumbi la maua (pollens) n.k.

 

DALILI UNAZOPATA UKIWA NA ALEJI

  • Kama ni mfumo wa hewa ndiyo ulioguswa, mtu anaweza kuwa na matatizo katika kupumua (kikohozi au kubanwa na pumzi, makamasi na kuziba kwa pua, muwasho kwenye pua na koo, au kupumua kwa kutoa sauti kama mtu anayepiga filimbi)
  • Kama macho yataguswa, muhusika hujihisi hali ya kuchoma choma, kutiririkwa na machozi na muwasho kwenye macho, macho kuvimba na kuwa mekundu.
  • Iwapo mtu atakula kitu ambacho ana aleji nacho anaweza kuwa na dalili kama vile kuharisha, kichefuchefu, kutapika, kusokotwa au kuumwa na tumbo.
  • Allergens zinazogusa ngozi zinaweza kusababisha ngozi kuwa na mabaka mabaka, kubabuka, kuvimba, muwasho, kuota vipele na malengelenge, michubuko au ngozi kuwa nyekundu.

Viashiria kwamba una aleji ya chakula hujionesha mapema zaidi, ndani ya dakika au masaa kadhaa baada ya kula chakula husika. Dalili hizi tunaziita allergic reactions ni kama:

  • Malengelenge yanayowasha kweye ngozi.
  • Mdomo kuvimba, kutetemeka na kuwasha
  • Ulimi kuvimba, koo na uso
  • Kutapika
  • Kuharisha
  • Maumivu ya tumbo
  • Kukohoa sana na mafua makali
  • Mwili kuchoka sana na kujiskia uvivu
  • Kupata ugumu kupumua ama pumzi kukata
  • Kupoteza fahamu

 

ALEJI INATIBIKA?

Njia bora kabisa ya kutibu na kupunguza uwezekano wa kupata aleji ni kutambua kitu au vitu vinavyokusababishia hali hiyo na kuviepuka.

 Kutibu aleji ya chakula na kupunguza madhara yake

Kutokana na kwamba aleji ya chakula inaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya, epuka kutumia vyakula vifuatavyo vinaongeza mpambano ndani ya mwili, kuzorotesha kinga ya mwili na kisha kuleta matatizo kwenye umeng’enyaji wa chakula.

Vyakula vyote vilivyosindikwa na kuhifadhiwa kwenye vifungashio visiharibike:

Vyakula vilivyosindikwa vimeongezwa kemikali, rangi na ladha vitu ambavyo vinaweza kusababisha aleji na mwili kushindwa kuvimeng’enya.

Sukari

Sukari husababisha ukuaji wa bateria wabaya kwenye mfumo wa chakula na hivyo kuzorotesha kinga yako ya mwili.

Vyakula vya ngano

Utafiti unaonesha kwamba watu wengi wenye matatizo kwenye mfumo wa chakula na matatizo ya aleji hupata nafuu kubwa na afya zao kuimarika pale wanapoacha kutumia vyakula vya ngano.

Usitumie vyakula vinavyoleta mzio/aleji kama;

Maziwa ya ng’ombe: Aleji kutokana na maziwa ya ng’ombe ni tatizo kubwa sana kwa watoto wadogo. Kwa watu wazima ni mara chache sana.

Mayai:  Mayai huleta mzio/aleji kutokana na uwepo wa kiini lishe kinachoitwa ovomucoid.

 

Tumia kwa wingi vyakula hivi ambavyo havileti aleji (allergic reaction)

Katika safari yako ya kupambana na aleji, fahamu kwamba kuna baadhi ya vyakula ambavyo havileti mpambano kati ya tishu za mwili na kinga ya mwili. Vyakula hivi ni kama;

Mbogamboga za kijani: Mboga hizi ni kama spinach ambazo zinakuwa na vitamin, madini, viondoa sumu, na viambata ambavyo husaidia umeng’enyaji wa chakua kwa wingi sana.

Maziwa ya nazi na nazi: Mbadala mzuri wa maziwa ya ng’ombe ni kutumia maziwa ya nazi.

Mbegu: Mbegu kama za maboga na mbegu za alizeti ni nzuri kwa mgonjwa wa aleji, huongeza madini ya zinc na mafuta ya Omega 3. Sawa na karanga, lakini uzuri wake ni kwamba hazisababishi mpambano (allergic reaction) ambayo huleta aleji au mzio.

Maziwa ya mama:  Tafiti mbalimbali zimethibitisha kwamba kunyonyesha mtoto kwa miezi sita ya mwanzo bila kula kitu chochote na kuendelea kunyonyesha kwa miaka miwili husaidia kupunguza hatari ya mtoto kupata pumu, matatizo ya ngozi na aleji mbalimbali.

Imeandaliwa na Mark Lewis






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post