Dili la kupika vitumbua vya nyama

Dili la kupika vitumbua vya nyama

Hali yako mdau wa Nipe Dili kila jumanne leo kwa furaha na shangwe zote nataka kukufundisha kitu adimu kabisa na sio wote wanaotambua ufundi huu nakuletea mezani sasa.

Enhee huu ni msimu wetu wa kupeana madili ya jikoni tu kuhakiksha tunazisaka hata ikiwa shilingi mia 500 sikuruhusu hasa kuipotezea ungana na mimi kweneye nipe dili leo nikifundisha namna ya kupika vitumbua vya nyama unaionaje hiyo?

I hope itakua imekaa poa sana na nimejua kukusuprse wiki hii karibu tuingie mzigoni sasa kama ifutavyo zingatia maelekezo ili uweze kutoa kitu kizuri kijana mwenzangu.

Tuanze na Mahitaji mwanakwetu haya hapaa!

Nyama ya Kusaga robo

Kitunguu maji 1 tu

Kitunguu thoum nusu kijiko kile cha chakula

Karoti yako 1 inatosha hasa

Pilipili hoho mambo yanukie jaman 2tu

Mayai 5-6

Baking powder nusu kijiko kidogo

Pilipili mbichi( ukihitaji lakini)

Usisahau na chumvi pia

Haya sasa twenzetu jikoni tuangalie namna  ya kupika vitumbua vya Nyama hatua kwa hatua.

Hakikisha umesafisha nyama yako vizuri itie vitunguu thoum, chumvi, pilipili manga na tangawizi, ibandike jikoni ili iive na ikauke vizuri.

Kisha kata kitunguu maji chako, hoho, pilipili, halfu vichanganye na mayai then vyote vitie kwenye nyama yako.

Weka kwenye Blenda mchanganyiko wetu usage kidogo lakini ili usiwe mlaini sana ukiwa tayari weka kwenye chombo ambacho unaweza kukaaa.

Baada ya hapo sasa weka baking powder, karoti na chumvi kidogo kisha changanya vizuri.

Enheee kisha andaa chuma cha kukaangia vitumbua bandika jikoni weka mafuta kidogo, mafuta yakipata moto chota rojo lako kwa upawa upo?

Utie kwenye kikaango vikiiva upande mmoja geuza na upande wa pili uive halafu uvitoe.

Sasa basi endelea kuchoma hadi viishe vyote hapo utakua umeshamaliza upishi wa vitumbua.

Bila shaka itakua tumeenda sawa bin sawia katika upishi wetu wa leo wish you all the best fighter wangu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post