Diddy agoma kula jela, tuhuma zaongezeka

Diddy agoma kula jela, tuhuma zaongezeka

Mwanamuziki kutoka Marekani ambaye kwa sasa anashikiliwa kwenye gereza la ‘Metropolian Detention Center’, Sean “Diddy” Combs ameripotiwa kugoma kula chakula anachopewa gerezani kwa kuhofiwa kuuawa huku tuhuma mpya zikiendelea kutolewa.

Taarifa hiyo imetolewa na aliyewahi kufungwa kwenye gereza hilo ambapo aliiambia runinga ya ‘News Nation’ kuwa chanzo chake cha karibu kutoka gerezani kimemwambia ‘rapa’ huyo amegoma kula chakula anachopatiwa gerezani hapo kwa kuhofia kuwekewa sumu.

Mbali na hilo mkuu wa zamani wa gereza hilo kupitia mtandao wa X alimpa tahadhari Combs, ya kuwa makini gerezani hapo kwani kuna wafungwa wanataka kumuua kama sehemu ya kuonesha ubabe wao pamoja na kupata heshima katika gereza hilo.

Mbali na hilo kupitia tovuti mbalimbali zimeendelea kueleza kuhusiana na tetesi kuwa Diddy amewekwa kwenye chumba cha uangalizi ili kuzuia kujiua licha ya mwanasheria wake Marc kudai kuwa mteja wake hana mpango wa kujiua.

Aidha nyota huyo ambaye amewahi kutamba na ngoma ya ‘Bad Boy for Life’ pia anakabiliwa na kesi nyingine ya kumi na moja ndani ya miezi 10 iliyopita ambapo anatuhumiwa kwa kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia mwanadada Thalia Graves tukio lililotokea mwaka 2001.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Rolling Stone’ Graves amedai kuwa Combs na mlinzi wake wa zamani aitwaye Joseph Sherman walimuwekea madawa ya kulevya, kumfunga mikono kisha kumbaka katika studio ya rapa huyo ‘Daddy's House’ iliyopo jijini New York.

Hata hivyo inasemekana kwamba baadaye Graves aligundua kuwa Combs alirekodi na kuuza tukio hilo kwa wachapishaji wa video za ngono mitandaoni huku sababu ya kuweka wazi kesi hiyo ni kudai fidia kutokana na madhara aliyoyapata.

Thalia Graves alikutana na Diddy kwa mara ya kwanza mwaka 1999, alitambulishwa kwa rapa huyo na mpenzi wake wa zamani ambaye alikuwa ni mtendaji wa zamani katika lebo ya Combs, Bad Boy na alikuwa akimtembelea mpenzi wake mara kwa mara kwenye studio za Diddy.

Ikumbukwe Diddy alikamatwa Jumatatu Septemba 16, na kuzuiwa katika gereza linaloitwa ‘The Metropolitan Detention Center (MDC) kwa tuhuma za ulaghai wa kingono na usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post