Baba amfunga binti yake CCTV kufuatilia mienendo yake

Baba amfunga binti yake CCTV kufuatilia mienendo yake

Baba mmoja kutoka Pakistan ambaye hajawekwa wazi jina lake amewavutia wengi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kumvalisha binti yake kamera ya ulinzi (CCTV) kichwani ili kufuatilia mienendo yake ya kila siku.

Wakati wa mahojiano ya binti huyo yaliyorushwa kwenye mtandao wa X, alieleza kuwa hilo lilikuwa wazo la baba yake na hakuwa na pingamizi kutokana na wazazi wake kuhofia usalama wake pamoja na kuepusha asifanye mambo ya ajabu.

Licha ya hayo pia binti huyo alifunguka kuwa sababu kubwa ya wazazi wake kuchukua uamuzi huo ni kufuatia tishio la ukatili dhidi ya wanawake huko Karachi nchini Pakistan.

Binti huyo anakiri kwamba baba yake anafanya kazi kama mlinzi wake wa kibinafsi kupitia mbinu hiyo isiyo ya kawaida kwa kufuatilia shughuli zake na mahali alipo.

Hata hivyo binti huyo alitoa wito kwa familia nyingine kufanya mbinu hiyo aliyoifanya baba yake kwani itawasaidia kutokuwa na hofu pindi watoto wanapokuwa mbali na nyumbani kwao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags