Ifahamu Nchi Yenye Watu 30

Ifahamu Nchi Yenye Watu 30

Kama ulikuwa hujui basi leo nakujuza zaidi, kuna nchi ndogo zaidi duniani iitwayo Molossia, ambayo imekuwa ikiwavutia wengi kufuatia na utawala pamoja na maisha ya wananchi wake licha ya kutotambuliwa rasmi na mataifa mengine au Umoja wa Mataifa.

Molossia au ‘The Republic of Molossia’, ni taifa dogo linalopatikana ndani ya jimbo la Nevada, nchini Marekani. Nchi hiyo ilianzishwa na Rais Kevin Baugh, ambaye pia ni mwanzilishi na mtawala wa nchi hiyo tangu mwaka 1977.

Taifa hilo lina jumla ya eneo la takribani hekari 0.055 tu (sawa na mita za mraba 550), huku ikiwa na wakazi waziozidi 30 ambao wengi wao wakiwa ni familia ya rais huyo.

Molossia linajitegemea katika vitu mbalimbali ikiwemo rais, katiba, Jeshi, Bendera na nembo, wanatumia pesa yao vilevile kuwepo na Sera za kigeni, na hata viza kwa wageni.

Aidha katika upande wa burudani Molossia ina Redio ya taifa (Radio Molossia) hupiga miziki mbalimbali na matangazo ya kiburudani, michezo ya ndani kama vile maonesho ya vipaji kwa wakazi. Mara nyingi rais wa taifa hilo ndio mtangazaji wa redio, mwigizaji na wakati mwingine hufanya vichekesho kwa ajili ya kuiburudisha jamii yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags