Utafiti: Watumiaji wa Iphone wanakiwango kidogo cha fedha na elimu

Utafiti: Watumiaji wa Iphone wanakiwango kidogo cha fedha na elimu

Wengi wanadhani kuwa watumiaji wa iPhone ni watu wenye fedha na elimu. Licha ya dhana hizo utafiti uliofanyika China ulibaini kuwa mawazo hayo ni tofauti na uhalisia.

Utafiti huo umebaini kuwa watumiaji wa Apple iPhone kwa ujumla wana kiwango kidogo cha elimu, wanakabiliwa na hadi duni ya kifedha, na wana mali chache zenye thamani, ikilinganishwa na watumiaji wa chapa nyingine za simu za mkononi kama Samsung, Xiaomi, Oppo, au simu zingine za teknolojia ya Android, kulingana na ripoti ya shirika la utafiti MobData.

Zaidi ya hayo, utafiti umebaini watu wengi wanaonunua iPhones ni wanafunzi wa vyuo vikuu, ambao wanazinunua kwa fedha zao za mfukoni, wengi wao wanatokea katika tabaka la kati. pia uligundua kwamba wengi wa watumiaji wa iPhone ni wanawake wasioolewa wenye umri kati ya miaka 18 na 34.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags