Aina tano za mavazi ya kiAfrika yanayovutia zaidi

Aina tano za mavazi ya kiAfrika yanayovutia zaidi

Habari msomaji wetu, ni siku nyingine tena tunakutana, imani yangu kuwa umzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kila siku ya kulijenga taifa.

Najua unafahamu kuwa kupitia kupitia page hii tunajuzana mambo mbalimbali ya urembo, mitindo, mavazi ambayo najua uwenda unayajua ila mimi nakujuza zaidi.

Leo napendwa kuwaalika kuangalia aina ya mavazi ya kiafrika yanayovutia zaidi ambayo ukivaa lazima upate muonekano mzuri na wa kuvutia.

Yapo mavazi matano ya kiafrika yanayovutia ambayo kwa hakika mwanamke unayependa kwenda na wakati ukiyavaa lazima utapendeza na kuvutia.

Kwa kawaida kila bara na kila nchi hapa duniani wamekuwa na aina yake ya mavazi asilia kama sehemu ya urembo na mitindo kiujumla.

Kwa upande wa urembo na mitindo asilia ya mavazi ndani ya nchi za ki Afrika kumekuwa na namna tofauti tofauti ya vitambaa, mwonekano, ushonaji na uvaaji. Yote hiyo ikilenga katika kuleta ladha ya kipeee ndani ya mwonekano wa mavazi.

Pengine kunaweza kuwa na aina nyingi ya mavazi asilia katika nchi za bara la Afrika lakini kwa upande wetu leo hii tunajikita zaidi katika kuelezea aina ya mavazi matano ambayo ni Kitenge, Batiki, Bazee, Makenzi na Khanga.

Kitenge

Kitenge ni aina ya vazi ambalo asili yake ni Afrika na matilio yake ni yenye uasili wa kudumu na kuvutia, kwa miaka kadhaa tangu lianze kutumika limekuwa likijipatia ubora na nafasi ya kipekee katika kukua na kuendelea zaidi.

Wanaume kwa wanawake wamekuwa wakishona mavazi ya kuendana nao na yamekuwa yakisasa na kufanya wawe wenye kuvutia.

Bazee

Vazi hili pia halina tofauti sana na kitenge katika sifa na ubora wake kwani vitambaa vyake vimekuwa vikipatikana kwa namna tofauti tofauti kuanzia ukubwa, rangi na maua yake yote hiyo ni kufanya muonekano wa kipekee na kuzidi kungara.

Batiki

Katika vazi hili uzuri wake huanza kuonekana pale baada ya kutengenezwa kwake kwa namna ya uchanganyaji rangi tofauti tofauti, ambazo mwonekano wake hujitokeza kama nakshi za maua maua.

Vazi hili pia umruhusu mtu yoyote yule kukidhi mahitaji yake ya aina au mtindo wa mshono ambao anauhitaji kwa muda muafaka.

Makenzi

Aina hii ya nguo kidogo kwa idadi ya watu wengi tuliozaliwa miaka ya hivi karibuni limekuwa geni kwetu japo sio sana. Kwani watu wengi hawavai sana vazi hilo hali iliyosababisha kizazi cha leo kutoliona zuri na lenye thamani.

Hata hivyo vazi hili limekuja kupata umaarufu na kuanza kujulikana na watu baada ya watu maarufu nchini kuanza kulivaa kwa kushona mitindo inayovutia.

Khanga

Vazi hili waswahili wamezoea kuliita jumba la fahari ya maneno hii ni kutokana na aina ya upambaji wake unavyo kuwa, maua yenye rangi tofauti tofauti, ukubwa unao jitosheleza mtu kujifunga au kushona na maneno yake yalivyo ambatana ndani yake.

Uzuri wa khanga inatoa nafasi nyingi kwa matumizi ya watu wote haswa wanawake. Kwa idadi kubwa ya maisha yao yote ya wanawake /mtoto wa kike hutumia vazi la khanga, kujifunga, kubebea mtoto, kushona na kazi zingine. 

Vile vile kwa upande wa mwanaume na mtoto wa kiume vazi hili linapata nafasi ya kutumika pale anapo pata tohara, kujifunga kwenda kuoga, pia hata kushona kama shati, kaptula na suruali.

Khanga inakupa uhuru sana kutokana na wepesi wa material yake yaliyoitengenezea ambayo inaifanya kuwa nyepesi inayo ruhusu kupitisha hewa na kuitumia kwa namna yoyote.

Huo ndio uasiri wa mwafrika katika mavazi ya asili yanayo wakilisha soko la urembo na mitindo duniani kote. Fahari ya mwafrika ni kujivunia katika kilicho bora.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post