Hakimi mchezaji wa Morocco alieibua hisia za wengi katika mitandao ya kijamii

Hakimi mchezaji wa Morocco alieibua hisia za wengi katika mitandao ya kijamii

Achraf Hakimi mchezaji aliyezaliwa Madrid ambae ameibua hisia za watu wengi katika mitandao ya kijamii, ameweza kuiondoa Uhispania kwenye Kombe la Dunia, nchi aliyozaliwa na kuipa ushindi wa kihistoria Morocco.

Achraf Hakimi alifunga penati ya ushindi na kuipeleka Morocco katika robo fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yao na kuigharimu Uhispania kutolewa katika mchuano huo.


Akifurahia ushindi wake Hakimi alikwenda hadi kwa kwa mama yake na kukumbatiana na kumpiga busu kwa mafanikio hayo

Hakimi ni mmoja wa raia wa Morocco wanaoishi nchini Uhispania, alikulia katika kaya ya kipato cha chini katika kitongoji cha Madrid cha Getafe.

Aliwahi kukaririwa akisema "Mama yangu alikuwa mfanya usafi na baba yangu alikuwa mchuuzi mitaani," alisema kwenye kipindi cha TV cha Uhispania, El Chiringuito.

"Walitoa maisha yao kwa ajili yangu walichukua vitu vingi kutoka kwa ndugu zangu ili nifanikiwe leo nacheza kwa ajili yao.” alisema

Morocco, timu pekee ya Kiafrika iliyosalia kwenye kinyang'anyiro hicho na imeweza imetinga hatua ya robo fainali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post