Travis Scott, Post Malone, Rema Kukiwasha Coachella 2025

Travis Scott, Post Malone, Rema Kukiwasha Coachella 2025

Tamasha la Muziki la Coachella linalotarajiwa kufanyika kwa wiki mbili April 2025, tayari wasimamizi wake wametoa orodha ya wasanii watakaoshambulia jukwaa hilo akiwemo Lady Gaga, Travis Scott, Post Malone na Green Day

Lady Gaga ameonesha kufurahia kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo

"Nimekuwa na maono ambayo sijawahi kutambua kikamilifu katika Coachella kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu lakini nilitaka kuja kwa mashabiki wa muziki. Nimekuwa nikitaka kurudi na kuifanya ipasavyo, na ndivyo. Ninaongoza na nikianza wikendi nikiwa Coachella. Siwezi kungoja kuwasikia nyinyi nyote na ngoma ya DANCE" aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram

Tamasha hilo la muziki na sanaa mbalimbali hufanyika kila mwaka katika Klabu ya "Empire Polo" huko Indio, California.likianzishwa na Paul Tollett na Rick Van Santen mwaka wa 1999, na limeandaliwa na Goldenvoice, kampuni tanzu ya AEG Presents.

Tukio hili linajumuisha wasanii wa aina mbalimbali za muziki, ikiwa ni pamoja na Pop, Indie, Hip-hop na muziki wa dansi, pamoja na uchongaji sanamu.

Coachella pia imetoa nafasi kwa wasanii wa Afrika kushiriki katika jukwaa hilo wakiwemo Rema (Nigeria), Tyla (South Afrika), Amaarae, na Sean Kuti ambao wote tayari wamethibitisha kutumbuiza katika tamasha hilo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags