Mbosso amuenzi King Kikii aimba Kitambaa Cheupe

Mbosso amuenzi King Kikii aimba Kitambaa Cheupe

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Mbosso amemuenzi nguli wa muziki wa dansi marehemu Boniface Kikumbi maarufu King Kikii ambaye alifariki dunia Novemba 15, 2024 kwa kuimba wimbo wa ‘Kitambaa Cheupe’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Khan amechapisha video akitumbuiza wimbo huo na kuandika kuwa ataendelea kumuenzi mzee huyo kupitia muziki wake.

“Pumzika kwa amani Mzee King Kikii vijana wako, watoto wako, wajukuu zako tutaendelea kuuenzi muziki wako ili tuendelee kujifunza mengi kupitia mazuri yaliyo ndani ya muziki wako, tutaendelea kuburudika na kujifunza kupitia muziki wako karne na karne”, ameandika Mbosso Khan

Ikumbukwe kuwa Joseph Silumbe ambaye ni mtoto wa marehemu 'King Kikii' aliweka wazi kuwa baba yake alifariki kwa maradhi ya saratani ya ini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags