Kazi za pamoja za wasanii hawa zinakubalika sana

Kazi za pamoja za wasanii hawa zinakubalika sana

Kuwa na muunganiko mzuri wa wasanii hufanya kazi zao kupendwa na kuwaletea mafanikio. Wengine hupenda kuita Duo ama Combo, wasanii hao wanakuwa sio kundi moja lakini mara zote wanapofanya kazi ya pamoja inateka masikio ya wasikilizaji.

Kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva kimebarikiwa kuwa na Duo au wasanii ambao wakikutana hufanya kazi nzuri leo tutawaangalia wasanii hao na kazi walizowahi kufanya

Roma na Stamina 'Rostam', kwa mujibu wa wasanii hawa kila wanapoulizwa kuwa wao ni kundi hukataa na kusema kila mmoja ni msanii ambaye anafanya kazi kivyake lakini wanapokutana kwa pamoja wanatambulika kama 'Rostam'. Wakali hao ambao wanatambulika zaidi kwa miondoko ya Hip-hop wamefanya kazi za pamoja kwa muda mrefu na kila wimbo wanaoachia ni mkali.

Walianza na "Hivi Ama Vile" iliyotoka Agosti 19, 2017 wakatambulika vizuri na duo yao ikapendwa zaidi badaye wakatoa ngoma zingine kama Kaolewa, Kiba 100, Hujambo Mwanangu, Kijiwe Nongwa, Watani Wa jadi, Kaka Tuchati, Parapanda na zinginezo.

Fid Q na Rich Mavoko, duo nyingine kali na pendwa kwa mashabiki ni hii ya Bandidu la Hip-hop "Fid" na "Messi" wa Bongo Fleva Richard Mavoko, wanamueendelezo mzuri wa kazi zao na zimekuwa na matokea mazuri ya kukubalika kwa mashabiki wa muziki.

Wana ngoma za pamoja kama Sheri,Tawile, Blow Up, BamBam, Mzandiki, na Champion. Kutokana na kukubalika kwa muunganiko wa wasanii hawa walitangaza kuandaa album yao ya pamoja ambayo bado haijafahamika itatoka lini

Belle 9 na G Nako, hii duo haikubahatika kufanya ngoma nyingi lakini kwa zile chache walizofanya zilithibitisha kuwa wao ni wakali wakifanya kazi kwa pamoja, Belle Tisa ni mkali wa R&B na G nako ni kama kiraka tu anafanya hip-hop, anaimba na vitu vingine.

Wamefanikiwa kufanya ngoma kadhaa kama Maole, Give It To Me na Kichaka ambayo walishirikishwa na mwanamama Saida Karoli kwa ngoma hizi ziliwafanya kukubalika zaidi kwa wafuasi wa muziki na hata walivyositisha kufanya kazi kwa kushirikiana iliacha maswali mengi kwa wadau wa muziki kwani wengi walitamani kuwaona wakiendelea kufanya pamoja

Diamond Platnumz na Zuchu, C.E.O wa WBC na Malkia wa lebo hiyo Zuchu hii nayo ni best duo inayofanya vizuri kila wakishirikiana kwenye kazi za pamoja ngoma lazima ziitike na mashabiki wakubali. Ukiachilia kudaiwa kuwa na mahusiano yao ya kimapenzi kwa kipindi fulani, kazi wanazofanya pamoja zinapokelewe vizuri ngoma kama Raha, cheche, Mtasubiri Sana, Litawachoma na zinginezo zinathibitisha hilo.

Ben Pol na Darassa, wamefanikiwa kufanya kazi nyingi na zote zimepokelewa kwa ukubwa, Ben Pol na Darassa wameanza kufanya kazi za kushirikiana kuanzia ngoma kama Sikati Tamaa, Show Off, Tatu, My Life na ngoma ya Muziki ya kwake Darassa ikitajwa kama moja ya hit za muda wote.

Taja Duo ya wasanii ambao wakikutana kufanya kazi unapenda zaidi?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags