Zingatia haya katika uuzaji wa nguo mitandaoni

Zingatia haya katika uuzaji wa nguo mitandaoni

Amkeniii amkenii amkeeni mkafungue biashara hizo, kama tunavyojua bwana biashara ni asubuhi kuna wale wateja wanaokuja alfajiri wanaboa kidogo lakini ndo ujasiliamali wenyewe huo.

Haya leo katika biashara tumeamka na wale wanaopenda kufanya biashara ya uuzaji wa nguo za jumla mitandaoni,

Kuuza nguo kwa jumla imekuwa ni biashara yenye faida ambayo inayokuwa kila mwaka. Kila mtu huwa anatafuta brand za nguo maarufu zinazouzwa kwa bei ndogo ambazo zitampatia faida.

Wauzaji wengi wana njia wanazozitumia siku zote kuuza bidhaa
Japokuwa soko la mtandaoni limekuwa ni njia rahisi sana kuuza nguo za jumla na soko linafanya vizuri mno kuliko hata watu waliotegemea.

Siku hizi utandawazi uko vyema sana na mitandao ya kijamii pia inafanya vizuri katika biashara, cha kufanya katika mitandao yako ya kijamii unachotakiwa kukifanya ni kuposti bidhaa zako tuu na sio vingine, na siku hizi unaweza kumlipa mtu ambae ana follows wengi akutangazie biashara yako na ukafanikiwa.


Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza nguo za jumla mtandaoni

  • Chagua aina ya nguo( trending dress)

Huwezi kumuhudumia kila mtu chagua aina ya nguo iwe moja au mbili tu unazotaka kuuza mtandaoni kama utambulisho wako kwa wanunuzi kama unauza magauni hakikisha ni magauni tu usichanganye na nguo nyingine lakini utofauti uwepo kwenye size ukawa na gauni za kuvaliwa na watu wote.

Mfano sasahivi watu wako katika mfungo wa kwalesma na waislamu wanatarajia kuuanza mfungo wao pia, cha kufanya kama unataka kufanya biashara hii angalia zile nguo za stara mfano mabaibui, sketi ndefu mitandio nk.

  • Nguo zilipotoka

Hapa Waambie watu nguo zako zinatoka wapi, ubora wa hizo nguo na brand ya hiyo nguo. Mfdano siku hizi watu wanapenda sana nguo kutoka Uturuki so ukiwaeleza umetoa huko itakuwa bora Zaidi kwasababu wateja wenyewe wanaamini kuwa nguo za huko sina ubora Zaidi.

  • Chukua picha za nguo zinazovutia

kwasisi wabongo bwana tunapenda kuona kile kinacho uzwa ndio tununue chukua kamera nzuri ya mbele na nyuma ya nguo
Pia piga picha ya maelezo yoyote ambayo yameprintiwa kwenye nguo
Hakikisha unachukua picha ya label yeyote ya nguo na picha ya maelezo kuonesha size ya nguo nk.

  • Tumia new model kuwaonyesha watu mavazi yako

Wateja wengi wanapenda kuona nguo imevaliwa na mtu harafu imemkaa vizuri ndo nayeye hutamani hapo hapo, sio lazima uchukue model ambao wanajuliakana ndo mana nikasema new hawa hawa ambao hawajulikani unaweza kuwatumia na biashara yako ikaendelea vizuri bila shaka.

Au unaweza kutazama nguo ulionunua je kuna mtu maarufu ameivaa ili uweze kuitangaza hiyo nguo kupitia yeye.

  • Pendelea kupost bidhaa zako mwisho wa wiki

Fatilia siku ambazo watu wengi wanakuwa online siku za weekend hasa jumapili watu wengi wapo online hii itakufanya uuze nguo kwa bei nzuri na watu wakakutafuta tofauti na ukipost bidhaa zako siku ya jumatatu au jumanne mtu anakuwa buzy na kazi na mambo yake mengine cha msingi posti nguo mpya kuanzia siku ya ijumaa mpaka jumapili.

  • Unganisha bei ya bidhaa na gharama za usafiri


Kuna baadhi ya wafanyabiashara mitandaoni wanaficha bei ya nguo na usafiri wanaposti tuu nguo, sasa hii haifai mwekee mteja kila kitu wazi na sio mpaka akupigie siku unaweza kukuta time hiyo mteja hana salio ay hajiskii kukutafuta DM lakini nguo anaitak.

Au kipindi unavyouza nguo zako utaweka bei ya juu ili kufidia gharama za usafiri lakini mteja atakapo kuwa anataka kununua bidhaa utamwambia usafiri ni bure

  • Mfanye mteja akumbuke huduma yako


Kila mauzo unayofanya hakikisha unakuwa na business card unaweza kuipata kwa bei rahisi na pia unakuwa na logo ili iwe rahisi mteja kukutafuta, au unaweza kubadilishana nae namba pindi utakapo kuwa unaposti nguo mpya aweze kuziona may be status nk.

Chingine cha kuongezea ni kumfanya mteja wako mfale, kuna siku nilikuwa nahitaji nguo mtandaoni nikapiga simu lakini yule muuzaji alinijibu kwa lugha ambayo sio nzuri, so jitahidi sana kuwa na lugha nzuri kwa wateja wako itakusaidia mno.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post