Jinsi ya kutengeneza vitumbua vya nyama kwa ajiri ya biashara

Jinsi ya kutengeneza vitumbua vya nyama kwa ajiri ya biashara

Amkeniii amkeniiii, unalala unamaisha amka tupambane ndugu yangu, lengo langu mimi kila week ni lile lile kukufungua wewe rafiki yangu ambae huna kazi au unakazi ila unahitaji upige pesa huku na huku.

Hapa nazungumzia biashara, ujasiliamali, kuchakarika leo katika mchongo wetu wa biashara nimekusogezea vitumbua vya nyama, najua utashangaa sana my wangu, kwa sababu ushazoe vitumbua vya mchele hapa unajionea mageni.



I hope itakua imekaa poa sana na nimejua kukusuprise week hii karibu tuingie mzigoni sasa kama ifutavyo zingatia maelekezo ili uweze kutoa kitu kizuri kijana mwenzangu.

MAHITAJI
• Nyama ya kusaga robo
• Kitunguu maji 1 tu
• Kitunguu saumu nusu kijiko kile cha chakula
• Karoti yako 1 inatosha hasa
• Pilipili hoho 2 mambo yanukie jamani
• Mayai 5-6
• Baking powder nusu kijiko kidogo
• Pilipili mbichi ( ukihitaji lakini)
• Usisahau na chumvi pia

Haya sasa twenzetu jikoni tuangalie namna ya kupika vitumbua vya nyama hatua kwa hatua.

Step 1: Hakikisha umesafisha nyama yako vizuri itie vitunguu saumu, chumvi, pilipili manga na tangawizi, ibandike jikoni ili iive na ikauke vizuri.

Step: 2 Kisha kata kitunguu maji chako, hoho, pilipili, kisha vichanganye na mayai then vyote vitie kwenye nyama yako.

Step: 3 Weka kwenye ‘blenda’ mchanganyiko wetu usage kidogo lakini ili usiwe mlaini sana ukiwa tayari weka kwenye chombo ambacho unaweza kukaaa.

Step: 4 Baada ya hapo sasa weka baking powder, karoti na chumvi kidogo kisha changanya vizuri.

Step: 5 Kisha andaa chuma cha kukaangia vitumbua bandika jikoni weka mafuta kidogo, mafuta yakipata moto chota rojo lako kwa upawa upo?

Step: 6 Utie kwenye kikaango vikiiva upande mmoja geuza na upande wa pili uive halafu uvitoe. Sasa basi endelea kuchoma hadi viishe vyote hapo utakua umeshamaliza upishi wa vitumbua.

Bila shaka hii imeenda sana, na kawaida yetu ni ile ile kama unatengeneza kwa ajili ya biashara inabidi kujaribu kadri uwezavyo mpaka uweze kutoa kitu sawia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post