Kufatiwa na machafuko kati ya Jeshi na kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF) huko nchini Sudani yamekuwa ya kiendelea takribani siku ya 3 mfululizo zaidi ikiwa katika mji mkuu wa Khartoum.
Aidha mashirika kadhaa yamesitisha huduma za ndege kutua nchini humo, Aprili 16, 2023, mapigano hayo ya kugombea utawala yalisitishwa kwa muda ili kuruhusu waliojeruhiwa kuhamishwa.
Nchi hiyo imekuwa ikiongozwa na majenerali tangu mwaka 2019 baada ya kupinduliwa kwa rais Omar al-Bashir ndipo mambo yakaanza kutokuwa sawa katika nchi hiyo.
Ingawa wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanasema chimbuko la mzozo wa sasa unarejea katika kipindi cha rais Bashir, ambaye alitawala nchi hiyo kwa takriban miaka 30 kabla ya kupinduliwa kupitia maandamano makubwa mwaka 2019.
Leave a Reply