Vitu muhimu kujifunza katika Teknolojia

Vitu muhimu kujifunza katika Teknolojia

Mapinduzi ya kiteknolojia ni kitu ambacho hatutaweza kukiepuka. Kadri dunia inavyobadilika, mambo mapya huvumbuliwa.

Leo nakuletea sehemu ya mambo machache muhimu yaliyoletwa na maendeleo ya technology na wewe kijana unapaswa kuanza kuviangalia kwa jicho jipya.

  1. CRYPTOCURRENCIES

Hizi ni sarafu za kidigitali zinazokuwezesha kuuza na kununua bidhaa huko huko mtandaoni. Ni aina mpya ya pesa, ila tu sio kama hizo tulizozizoea kuzishika. Moja ya sarafu kubwa zaidi duniani ni ile ya kwanza kabisa iitwayo Bitcoin. Ni muhimu sana kwa kijana kujifunza zaidi juu ya sarafu hizi kwani biashara nyingi mpya za mitandaoni kama vile NFTs hulipiwa na sarafu za kidigitali pekee.

  1. METAVERSE

Nadhani tulishawahi kuzungumzia kuhusu hili katika makala za nyuma. Metaverse ni kitu ambacho kilikuwa kimetabiriwa kuja kwa miaka ijayo, na sasa imefika kwa speed, ikiwa kampuni kubwa kama FaceBook imeamua kuinvest mazima katika hili kupitia kampuni yao ambayo sasa inaitwa META.

Kwa kiufupi, Inamaanisha ni kwamba badala ya kushirikiana na marafiki wako mkondoni kama ilivyo sasa, unaweza kukutana nao katika ulimwengu wa dijiti katika avatari zako za dijiti, ukitumia kichwa cha habari halisi au kifaa kingine.

Awali haya mambo yalikuwa yanaonekana kwenye movie tu, tena zile zilizojaa uongo, little did we know haya yatakuwa reality ndani ya muda mfupi.

  1. NFTs

Hii kwasasa ndio “hot cake”, yaani habari kubwa mjini. Vijana wengi wenye uelewa wameanza kujifunza kuhusu hili. Hii ni tokens zisizofungamana, yaani zile ambazo ni unique na zinauzwa kupitia market zake special, ambapo unaweza kuuza na kununua bidhaa ya kidigital kwa kupitia cryptocurrencies.

Watu wengi wamekwisha pata faida za juu kutokana na hili na moja kati ya famous NFTs ni collection ya Bored Ape ambapo mastar wakubwa duniani kama vile Dj Khaleed na Neymar wamenunua picha hizo.

Kama wewe ni creator basi hii ni nafasi nzuri ya kuingia katika hili, lakini hata kama hauna chembe za creativity ndani yako, unaweza kununua bidhaa na kuresell ila tu, creator atapata royalties zake katika kila mauzo ya hiyo bidhaa.

  1. AUTOMATED CARS

Nani alidhani kwa sasa tutakuwa na magari yanayotumia umeme, magari yanayojiendeshe na hata magari yanayogeuka kuwa ndege na kupaa?

Hiyo ndio raha ya technology. Makampuni makubwa kama Tesla ndio waasisi wa hii teknolojia ambayo kwasasa ina shika kwa kasi mno.

African countries better watch out kwani vitu kama “Aircar” vikifika itakuwa tafrani…. Bye bye foleni, barabara ikizingua, gari lageuka ndege TUNAPAA.

  1. HUMAN BRAIN CHIP

Hivi karibuni hapa hapa Tanzania nasi tumezindua project katika hili lakini cha msingi ni kwamba, hizi ni chip zinazowekwa kwenye ubongo wa binadamu, ambapo itamsaidia kupata majibu ya maswali kwa uharaka, na hata majuu wameenda mbali kwa kupandikiza watu wenye ulemavu wa mwili ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Kweli dunia imebadilika mno na ukikaa kwa kuzubaa, basi muda si mrefu itakupita. Hakikisha unajifunza zaidi juu ya haya kwani ukifanya vizuri, faida yake ni nono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post