Vazi la kitenge linavyo endelea kubamba

Vazi la kitenge linavyo endelea kubamba

Hellow!! Guys mambo zenu mimi najua ni wazima kama kawaida yetu sisi tupo kukusogezea yale yote yanayobamba katika mitaa ya fashion na urembo, kama wanavyosema waswahili jasiri aachi asili wiki hii sasa ni kivumbi.

Leo katika fashion tuna kitu kingine kipyaaa japo tunayo mengi ambayo tulisha kugusia ila na hili nalo vazi la kitenge hatuachi lazima tukwambie, ni vazi ambalo mababu na mabibi zetu walilitumia kabla ya hivi vitambaa vya hariri na shifoni tunavyo vishona.

Wengi wetu tuna fahamu vitenge na haswa kwa sisi Waafrika sio kitu cha kushangaa kabisa, kitenge ni miongoni mwa mavazi ya kiafrika yenye heshima ya kipekee  na ni moja ya vazi linalo watambulisha waafrika kutokana na uhalisia wake.

Vazi hili nitofauti na mavazi mengine au mitindo mingine kama vitambaa, kitenge kina sifa yake ya kuvaliwa na watu tofauti tofauti na huleta maana kwenye fashion.

Sasa katika kuonyesha thamani yake wabunifu wa fashion wameenda mbele zaidi na kubuni hadi mapambo ya kitenge hivi karibuni imekuwa sijambo la ajabu kuna hereni, bangili,mikoba na hata viatu vya kitenge.

Kwa miaka kadhaa imethibitika kitenge kikivaliwa katika mitindo kadha wa kadha kwa mfano magauni, makoti, blauzi na sketi.

Yaani kadri siku zinavyozidi kwenda mitindo ya vitenge ya aina mbalimbali imekuwa ikibuniwa, ubunifu huu umekuwa ukiongeza thamani zaidi ya kitenge na hata kukubalika na kufahamika ndani na nje ya Afrika.

Kwa taarifa yako tu labda nikwambie kuvaa kitenge kunatosha kabisa kuonyesha kwa jinsi gani unajali na kulinda utamaduni wako mfano Nigeria wanaongoza kwa kuvaa mavazi ya vitenge wakiwakilisha utamaduni wao.

Lakini kama ilivyo kwa nchi nyengine kama india kwa kidumisha utamaduni wao kwa kuvaa sari kama tunavyojua ndo vazi lao maarufu sana na kwa Afrika naweza kusema vazi la kitenge nitamaduni yetu.

Kwa kipindi hiki wabunifu wamebuni mashati ya kiume ya vitenge tena kwa mitindo tofauti na kabla ya kuyaingiza sokoni hupitishwa katika maonyesho kadhaa ya mitindo ili kufahamu jinsi ya uvaaji wake.

Leo hii imeweza kueleweka katika jamii kuwa vazi la kitenge linaweza kutengeneza shati kwa upande wa wanawake na wanaume wanaweza kuvaa katika sehemu mbali mbali kama vile ofisini kwenye sherehe nk.

Sambamba na hayo team ya Mwananchi Scoop iliweza kufika mpka Sinza makaburini kwafundi na muuzaji wa vitenge anajulikana kwa jina la Halima Ndembo ambapo alituelezea mambo wakadha kuhusiana na vazi hilo la kitenge na kueleza kuwa alianza kwa kuuza vitenge tuu na  alivyoona wateja wake ni wengi akaamua ajifunze kushona so akawa ana washonea…

“Siku hizi vitenge vina mitindo mingi ya kuvaa mwanzoni wateja wangu walikuwa wanawake peke ake sasahivi hadi wanaume na ndio wamekuwa wateja wangu sana kushinda wanawake kwa sasa”alisema Halima


Mahali ambapo anafata bidhaa hizo ni nchini Congo na wakati mwengine oda zikimzidi huwa ana budi kuchukua katika maduka ya jumla ili kuokoa muda.

Pia wateja kwake wanafurika tofauti na alivyo anza kwasababu ya kuwauzia bei nafuu na wengine kuwashonea hapo hapo na mara nyingi wateja wake huchagua mishono tofauti tena ya kisasa.

Halima amezungumzia changamoto anazokumbana nazo katika biashara yake hiyo na kueleza kuwa “kuna wateja wanakuja na mishono tu ambayo wameiona mtandaoni wanataka uwashonee kama huo mshono unajua si kila mshono utampendeza mteja hapo ndipo napo kuwa pagu sana kifupi mteja hataki umshauri na asipo pendeza anakulaumu hujui kushona” alisema Halima

Kama kawaida katika kila biashara lazima kuwe na faida hata kama ni shiringi mia mbili, kwa upande wa mwanadada huyo yeye alisema kuwa amepata mafanikio makubwa katika biashara yake ya kuuza vitenge na kushona kuliko hata alivyo tegemea.

Team ya Mwananchi Scoop haikuishia hapo tu kwa mara nyengine ikakutana na mama mjasiria mali Bi Mwanaisha Mpoki mkazi wa Kilungule Mbagala yeye anasema huwa anachukua vitenge kigoma na kuviuza katika maofisi na watu wengine wa mtaani japo wateja wake wakubwa ni wafanyakazi.

“Mimi kwanza ndio biashara ninayo itegemea na nilianza kuitangaza katika ofisi mbalimbali nikaona muitikio mzuri na kwakweli vitenge vina valika sana hususani na vijana tofauti na zamani ilizoeleka kuvaliwa na ila saivi ni tofauti” ameyasema hayo Mwanaisha

Kwaupande wa changamoto katika biashara yake anaeleza kuwa kunakipindi biashara inakuwa sio nzuri kwasababu wateja wake wanakuwa ni walewale.

 “Sio kila siku utapata mauzo mazuri kutokana na wateja wangu mimi niwasikuzote so kuna muda wanakuwa hawana uhitaji navyo hiyo ndo changamoto yangu kubwa ”alisema majasiria mali huyo.

Aidha vitenge vimekuwa na uhitaji mkubwa mpka kutoka kwenye tamaduni hadi kwenda kwenye fashion, siku zote waswahili wanasema mcheza kwao hutunzwa so tusiache asili yetu kwa mavazi ya kupita.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post