Urusi, marufuku kutaja mapenzi ya jinsia moja

Urusi, marufuku kutaja mapenzi ya jinsia moja

Bunge dogo la Urusi limepiga kura kwa kauli moja kuongeza marufuku yake kwa kile kinachoitwa "propaganda za mapenzi ya jinsia moja".

Chini ya toleo la hivi punde la sheria, uendelezaji wowote wa maudhui ya wapenzi wa jinsia moja - ikijumuisha katika vitabu, filamu na mtandaoni - ni kinyume cha sheria na hubeba adhabu nzito.

Hii ni sheria iliyopewa jina la utani la "Jibu kwa Blinken", na ni baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kuikosoa kama "pigo kwa uhuru wa kujieleza".

Sheria hiyo Iliidhinishwa kwa kura 397 huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja aliyepinga.

Muswada huo bado unapaswa kupitishwa katika baraza la juu na kutiwa saini na Rais Vladimir Putin, lakini hii inaonekana kama hatua ya kiutawala.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post