Waswahili husema mcheza kwao hutunzwa, hivi ndivyo lafudhi ya Kimakonde ilivyobadili maisha ya Tabu Mtingita mzaliwa wa Mtwara kuwa miongoni mwa waigizaji mahiri nchini Tanzania.
Tabu ambaye aliingia kwenye uigizaji akiwa na umri wa miaka 40 ameiambia Mwananchi Scoop mwanzoni haikuwa rahisi kuingia katika tasnia hiyo.
“Kwanza kabisa haikuwa rahisi kama watu wanavyodhani mimi kuingia katika sanaa ya uigizaji japo nilikuwa napenda sanaa lakini kwa bahati mbaya wazazi wangu walikuwa hawataki kabisa nijihusishe na masuala hayo” alisema Tabu.
Hata hivyo ameeleza jinsi wazazi wake walivyokuwa wakimuwekea matarajio katika elimu, ambayo amedai hakuwa na akili ya darasani hivyo alijikuta akirudia darasa zaidi ya mara tisa.
“Mimi bhana sikuwa na akili nilivyokuwa shule, japo wazazi wangu walijitahidi kunisomesha. Kwa sababu walitaka nikae ofisini lakini nilivyokuwa kidato cha nne niliambulia ziro licha ya kurudia darasa mara tisa” . Alisema.
.
.
.
#Mwananchi Scoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply