Smart Jay na Matamanio ya kuwa commedian anayeheshimika

Smart Jay na Matamanio ya kuwa commedian anayeheshimika

Na Aisha Lungato

Name; John Lucas

Birthday; November, 12

Kazi; Student & Comedian

Nasemajeeee! Mwananchiscoop isipotoka this Friday niite Mbwa niko nimekaa pale, hahahaha nafikiri wanangu nikizungumza hivi mnanielewa, ile segment yetu ya kujua mawili matatu imemnasa kijana mmoja hivi ambaye ametrend vibaya mno kwa kauli yake ya ‘niite mbwa’.

Kama tunavyo semaga kuwa hatunaga mba mba mba leo tumepiga na mwamba huyo na kutueleza mawili matatu kumuhusu, kwa majina kamili anaitwa John Lucas ni  mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) kozi ya Food Science and Technology wengi wenu mnamfahamu kupitia jina la Smart Jay au ‘Niitembwa’ jini hili ambalo limebeba dhana halisi kupitia clip yake ambayo inafanya vizuri sana katika mitandao ya kijamii tofauti tofauti.

Changamoto anazo kumbana nazo kupiti uchekeshaji

Smart Jay alifunguka kuhusiana na changamoto anazo zipata katika kufanya kazi zake hizo na kueleza kuwa “changamoto ya kwanza ni kukutana na watu wenye perception tofauti tofauti pili ni kukutana na watu wanaojifanya wanajua sana sheria wanakusumbua na wanaweza hata kukuletea shida yani kitu ninacho kifanya mimi ni kama risk inaweza kusababishwa hata kupigwa” Amesema Smart Jay

Matamanio yake katika tasnia hii ya uchekeshaji

kama tunavyo jua katika kila mwanadamu anamatamanio yake ya kufika sehemu fulani ndiyo mana wengi wao wana struggle ili kufikia matamanio yao kwa upande wa Jay yeye alieleza kuwa “ Nikiwa kama mchekeshaji matamanio yangu makubwa ni kuwa comedian anaeheshimika ukiweka listi hata niwe kati ya top 10 sio mbaya pia natamani niwe comedian ninaetengeneza pesa kupitia kipaji changu” Amesema John Lucas

Maisha ya mahusiano

Ooooooh! Siku hizi waswahili wanakamsemo kao katika marriage status kuwa Jimbo liko wazi halina mgombea kwa upande wa Niitembwa au Smart Jay yeye anasema bado yuko single   anapambana kwanza atoboe mengine ndiyo yaweze kufuata, yeye bwana hana mapenzi ya Harmonize hahahaha jokes bwana.

Historia fupi ya Niitembwa

John Lucas ni mtoto wa kwanza katika familia yao na amezaliwa Mwanza na amekulia mkoa wa Tabora Wilaya ya Nzega katika kijiji cha Bukeni na level yangu ya elimu kwasasa bado mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Historia yake ya uchekeshaji ilipoanzia

“ Comed mimi nilianza o level lakini Moshi Technique niliongeza juhudi zaidi mana nilikutana na rafiki ambaye naye yuko na interest katika kitu hicho tukawa tunafanya comedian like burudani tuu nafsi zetu zilizike na watu wacheke basi, lakini tulivyo fika chuo tukaamua kufanya uchekeshaji kama biashara ya kuwa njia yasisi  kupata pesa” Ameseama Smart Jay

Binadamu wote hatuwezi kuwa sawa kwa mambo ambayo tunayapenda na tusio yapenda kwa upande wa bwana mdogo Jay alifunguka na kueleza kuwa “ Vitu ninavyo vipenda ni respect, kujituma na kuishi kwa amani kuheshimiana na kila mmoja sio mkubwa wala mdogo na mambo nisiyo yapenda jambo kubwa zaidi ni dharau” Amesema John

“Chingine ambacho naweza kuongezea ambacho ni kitu nahitaji watu wajue ni kwamba everything hapen for are reson hata kama ni kitu kibaya vipi kimekutokea basi kimetokea kwasababu ya mungu, kwenye Maisha yangu mimi kuna vitu vibaya vingi vimenitokea lakini kupitia hivyo hivyo vitu vibaya vikaja vitu vizuri zaidi ambavyo sikuwahi kuvitegemea sio watu wasikate tamaa tuendelee kupambania ndoto zetu mimi maamini Mungu wetu anatusikia wote tupambane kwa ajili ya ndoto zetu ilimradi tusivunje sheria za nchi wala amri za Mungu” Amesema John Lica

Kupitia Mwananchiscoop Jay amefunguka kuhusiana na project yake mpya na kueleza kuwa “Kwanza niwashukuru wote mlionipokea kwakweli mmenipa nguvu ya kufanya kazi zaidi kwa mapokezi yenu ya upendo, kwanza mashabiki zangu nataka mkae mkao wa kula nakuja na vitu konki msiache tu kufuatilia mitandao yangu ya kijamii ili msipitwe” Amesema Samrt Jay

We love Smart Jay because firstly he is a young man and he does well through his comedy   he knows how to miss it and give the community something they love, so we advise budding comedians to follow in John footsteps in order to be Comedian successful.

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post