Simulizi: Kwa Udi na Uvumba..!

Simulizi: Kwa Udi na Uvumba..!

 

Na Innocent Ndayanse(Zagallo)

NI usiku wa manane. Saa saba! Kwa wapenzi hawa wawili, bado ilikuwa mapema sana. Walikuwa hawajaambulia hata lepe la usingizi. Na zaidi, ni Hilda aliyekuwa akitaabika kwa kukikosa kile alichokihitaji, kile ambacho huukonga moyo wake kwa namna inayosisimua na kufariji.

Tayari alikwishaitumia mikono kugusa hapa na pale, kutomasa na kupapasa huku na kule lakini haikusaidia. Akayatumia matiti yake makubwa yenye joto la uhai, haikusaidia. Alitumia hata ulimi wake kitaalamu na kwa mbwembwe nyingi; lakini bado ni kama alikuwa akipoteza muda!

“Una nini leo?” Hilda alitokwa na swali hilo huku akiuondoa kwa taabu mkono wake ambao kwa dakika mbili, tatu ulikuwa mahala fulani mwilini mwa Panja, ukiendelea kujaribu kuyashtua mashetani.

“Kwani vipi?”

“Hii siyo kawaida yako.”

Ni kweli, hiyo haikuwa kawaida ya Panja kila arudipo jioni kutoka katika safari zake ambazo Hilda hakuzijua. Alishajenga mazoea ya kila aliporejea huvuta bangi na kunywa pombe kali kidogo.  Kinachofuata  baada ya hapo ni ile adhabu yenye kusisimua maungoni mwa Hilda, wakitumia muda mwingi wa usiku huo kufanya hicho walichozoea kukifanya.

Lakini usiku huu Panja alikuwa mwingine. Alionekana kutingwa na mawazo mengi kichwani, mawazo yaliyosababishwa na mkasa uliomkuta katika safari yake aliyorejea mchana uliopita.

GEREZA la Segerea lilipompokea Panja na kumpa hifadhi ya miaka miwili kwa kosa la wizi wa kuaminiwa, alipata mafunzo mengi ambayo hakuyatarajia. Kati ya mafunzo hayo ni machache tu aliyoyapenda. Alitoka huko akiwa ameshajua kuvuta bangi. Zaidi ya hayo, marafiki zake aliokumbana nao huko walimpa mbinu mbalimbali za kupata fedha kwa njia za haraka na fupi.

“Wenzio tumeingia humu kwa sababu za maana,” Makata, mmoja wa wafungwa wakongwe alimwambia. “Tulikuwa wanne, tukamvaa bwege mmoja wa Kihindi, tukamlisha za kichwani na kutoka na milioni ishirini. Tatizo, mnoko mmoja aliwatonya ‘wazee,’ tukataitiwa kabla hata hatujakatiana mshiko.”

Mwingine alimwambia kuwa atakapotoka kifungoni atakuta milioni zake tatu katika akaunti yake, benki. Yeye alidai kuwa alihukumiwa miaka mitano jela baada ya kutuhumiwa kuvamia nyumba ya jirani  na pale alipoishi, tuhuma alizokiri kuwa ni za kweli.

Kipanga, mfungwa aliyekuwa amebakiza wiki moja tu za kutumikia kifungo, yeye, japo aliwasikia wenzake wakitamba, hata hivyo hakutamka chochote bali baadaye alimwita Panja faragha na kumuuliza, “Hivi wewe umebakiza miezi mingapi?”

“Siyo miezi, ni siku kumi na tano tu.” 

“Wiki mbili tu!” Kipanga alimtazama kwa mshangao. “Kumbe siku zimekwisha! Nilidhani bado una siku nyingi, kumbe…”

Ukimya wa sekunde kadhaa ukatawala. Kisha Kipanga akaendelea, “Kumbe hatupishani sana. Mie bado siku saba tu. Nitakutangulia wiki moja.”

Panja hakumwelewa. Kwa sauti yenye kijimkwaruzo cha mbali, alimuuliza, “Kwa hiyo nd’o nini?”

Kipanga alicheka kidogo, kisha akasema, “Kuna jambo unalopaswa kulijua msh’kaji wangu. Kwamba, umesota humu kwa ‘mvua mbili’ kwa kosa la kipuuzi. Utafanya nini utakaporudi uraiani?”

“Hilo nitalijulia hukohuko,” Panja alijibu. “Kama maisha ya Bongo yatanishinda, basi nitazamia majuu.”

Kwa mara nyingine Kipanga alicheka, safari hii kicheko chake kikionyesha kuyadharau maneno ya Panja. “Utazamia?” hatimaye alimuuliza. “Una akiba ya nguvu, benki?”

“Sina. Lakini n’tafaiti hukohuko uswazi.”

“Una hakika na unachokisema?”

“Sina. Mambo yote n’tayajulia hukohuko.”

“Siki’za, Panja,” Kipanga alisema kwa sauti ya chini. “Unaonekana uko fiti kishenzi. Umbo lako linafaa kutumika katika kukunufaisha. Siku hizi maisha ni magumu. Ili ufanikiwe usitegemee kukesha kanisani au msikitini ukisali. No. Mwanaume unapaswa kuhangaika. Fanya kila liwezekanalo, na kulazimisha uwezekano kwa lile lisilowezekana ili ufanikiwe maishani. Tangu uzaliwe u’shawahi kupiga mtu roba?”

“Bado,” Panja alijibu kwa sauti ya chini huku akimkodolea macho Kipanga. Hakutarajia kuulizwa swali hilo.

“Wewe bado, mie tayari. Na siyo kupiga mtu roba tu, mwanangu. Mi’ ni’shazimisha mtu nne, kudadek! Na sikufanya hivyo kwa kujifurahisha tu. Hapana. Nilikuwa na sababu. Pesa. Nilitaka pesa, na nilizipata. Nikajenga. Najua nikitoka humu nitafikia nyumbani kwangu siyo kuhaha tena mjini. Kwa kweli huo ndio mfumo wangu wa maisha. Na nikitoka humu kazi yangu ni hiyohiyo. Lakini nahitaji kampani. Mtu kama wewe nd’o anayefaa kunipa kampani, mwanangu. Chimbo langu liko Kariakoo maeneo ya Jangwani, jirani na jengo la  Yanga. Siku n’takayosepa n’takumwagia vizuri jinsi ya kunicheki.”

Itaendelea……….

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post