Baada ya mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano ya Euro kati ya wenyeji timu Ujerumani dhidi ya Denmark kumalizika, polisi waliokuwa wanalinda uwanja walimshusha shabiki mmoja aliyefanya vurugu kwa kuapanda kwenye paa lililokuwa linafunika jukwaa .
Mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa BVB Dortmund, baada ya kumalizika kwa Ujerumani kushinda mabao 2-0, polisi walionekana wakijongea eneo lililokuwa na lundo la mshabiki ambapo waliwatawanya ili kupita kwenda kumshusha shabiki huyo aliyevalia kinyago cha kuziba sura.
Tovuti ya Dail Maily imeeleza kuwa mwanamume huyo alitembea juu kenchi za paa hilo, huku mashabiki waliokuwa wakitazama tukio hilo wakimpigia kelele kwamba ashuke.
Tukio hilo linadaiwa kuibua wasiwasi wa kiusalama kwa mashabiki wakati michuano hiyo ikiendelea.
Wiki iliyopita, UEFA ilitoa taarifa ambayo ilieleza, usalama katika viwanja vya mechi za michuano hiyo utaimarishwa zaidi baada ya kutokea kwa matukio kadhaa ya mashabiki kuvamia uwanja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply