Mamlaka ya jiji la Eldoren nchini Kenya imeondoa sanamu la wanariadha Eliudi Kipchonge na Faith Kipyegon waliyoiwakilisha nchi hiyo katika mashindano ya Olimpics 2024 jijini Paris Ufaransa.
Sanamu hizo zimeondolewa kufuatia malalamiko ya wananchi kuwa sanamu hizo hazifanani kivyovyote nani dhihaka kwa wanariadha hao.
Faith (30) ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu upande wa wanawake, katika mbio za mita 1500 alitumia dakika 3:51.29 na kumfanya kuwa mwanariadha wa kwanza wakike kushinda medali tatu za dhahabu katika mashindano hayo ya Olimpics.
Katika mashindano hayo ya Olimpics mwanariadha Eliud kipchonge (39) alishindwa kumaliza mbio za kilomita 30 kwa kile kilichotajwa kuwa ni maumivu ya mgongo baada ya kukimbia kilomita 20.
Bingwa huyo mara tano wa Berlin Marathon alishinda taji lake la kwanza la mbio za Marathon katika michezo ya Olimpics ya Rio 2016 kabla yakutetea taji lake katika michezo ya Olimpics ya Tokyo 2020 na kushinda medali ya dhahabu kwakutumia muda wa 2:08:38 ambapo mshindi wa pili alimaliza mbio hizo baada ya sekunde 80.
Kwa ushindi huu Kipchonge anakuwa watatu kuvunja rikodi ya kushinda mbio za Olimpics mfululizo huku akitanguliwa na Abebe Bikila wa Ethiopia alieshinda kwa mfululizo huo inchini Rome mwaka 1960 na Tokyo 1964 alikini pia Waldemar Cierpinski vivyo hivyo huko Montreal,Canada 1976 na Moscow 1980.
Leave a Reply