Sababu tano zinazofanya wasanii wa bongo fleva kupotea kwenye game

Sababu tano zinazofanya wasanii wa bongo fleva kupotea kwenye game

Wanangu niaje? Its another Friday, siku zinakata kama upepo na bila kupoa  tunazitafuta na kuzikusanya habari zote za burudani na kukusogezea mwanangu wa faida ndani ya jarida lako pendwa la Mwananchi Scoop.

Ebwana kwa wale ambao walikosa makala ya week iliyopita ndani ya jarida la Scoop katika kipande hichi cha burudani tuliangalia mastaa wa muzikii wa Bongo Fleva waliotamba katika game kwa miaka ya 2000. Wasanii hao licha ya kutambaa na ngoma kalii pia walijizolea umaarufu na tuzo za ndani na nje ya nchi kupitia talanta ya muziki na miongoni mwao ni wakina Juma Nature, Chid Benz, Lady Jaydee Ray C na wengine wengi.

Basi bhana baada ya kuzungumza na wadau tofauti tofauti katika tasnia ya mzuiki kuhusiana na sababu zinazosababisha wasanii wa bongo fleva kupotea kwenye game ilihali wana muziki mzuri na ngoma zao zinadunda kitaa, wadau hao walifunguka yafuatayo kuwa ndo sababu zinazosababisha wanamuziki wa bongo fleva kupotea kwenye game nazo ni:-

 

·      Wasanii kutokuwa na vipaji asilia vya uimbaji

Wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya wamekuja katika sanaa kupambana na hali ngumu ya maisha hivyo wengi wao hawana asili ya Sanaa. Ukiangalia hata historia zao hivyo utagundua sanaa sio kitu chao na kushindwa kufanya ubunifu au kufanya kazi zao kwa mihemko au mkumbo.

Hivyo kupelekea wasanii hao kutodumu katika tasnia ya muzikii baada ya kutoa ngoma mbili tatu kisha kuachana na muzikii pia hata kuendelea na sanaa nyingine.

 

·      Ukosefu wa elimu kwa baadhi ya wasimamizi wa wasanii.

Wasimamizi wengi wa muziki wa hapa nyumbani hawana uelewa mpana namna ya uwekezaji katika tasnia hii.

Meneja wengi huwa ni watu wasio na taaluma ya sanaa hususani katika kuifanya tasnia hii kuwa biashara na miongoni mwao hudhani muziki ni kurekodi na kufanya shows za ndani na nje ya nchi na kusahau  kuhusu kuwekeza katika kuboresha maisha ya  msanii ili kumpatia utulivu wa akili ambapo itamsaidi kufocus katika kazi vizuri jukwaani pia kurekodi nyimbo nzuri ambazo zitamtangaza msanii kimataifa.

Vilevile msanii anatakiwa kuwa na timu ambayo itamsimamia kwanzia utayarishaji wa muzik,i kurekodi, mtu wa kumtafutia interview kwenye vyombo vya habari na  kumtafutia watu wa kufanya nae collabo pia   kumtafutia au kubuni matamasha ambayo yatamsogeza msanii karibu na mashabiki na wadau tofauti wa muziki.

·      . Vyombo vya habari

Pia ni moja ya sababu inayosababisha wasanii kupotea kwenye game ukizingatia muziki umekuwa biashara hivyo kufanya baadhi ya vyombo vya habari kuanzisha matamasha katika kujiongezea kipato.

Aidha baadhi ya wasanii kulazimishwa kufanya tamasha kwa malipo madogo au kutolipwa kabisa kwa kigezo cha wimbo wake kupigwa redioni na kama msanii akigoma kuperform kwenye hayomatamasha yaliyoandaliwa basi nyimbo zake husitishwa kupigwa redioni na msanii kupotea ama kusahaulika kwa mashabiki.

Hii hupelekea msanii kushuka kimapato vilevile matamasha haya husababisha msanii kuwa na jina kubwa na kutokuwa na kipato cha kuweza kuendesha shughuli za kisanii.

·      Wasanii kutokuwa na msimamo

Wasanii wetu wengi hawana msimamo katika aina ya muziki inayowatambulisha kama walivyo wasanii wa kimataifa katika Hip Hop, R&B, Ragger au soul nk.

Wasanii wa bongo hawana utambulisho rasmi katika aina za muzikii na wengi hurekodi muziki kulingana na aina ya muziki uliopo kwenye soko ili kwenda sawa na wakati ambapo husababisha msanii kupotea mara tu aina hiyo ya  mzuiki ukipotea.

Kwa mfano katika kipindi hiki, wanamuziki wengi wamehamia kwenye aina ya mziki wa amapiano na kusahau aina yake ya muziki uliomtambulisha kwa mashabiki.

·      Tabia binafsi

Kuwepo kwenye muziki au kutokuwepo hutegemea pia tabia binafsi ya msanii kama kioo cha jamii.Kuna ambao huchukiwa tu na mashabiki kutokana na tabia zao wanazozionesha wanapokuwa mbele za mashabiki au hata katika maisha yao ya kila siku.

 

Pia vitu kama kutojituma, kuvimba kichwa kutokana na mafanikio ya sanaa yake, ufedhuli, ulevi wa kupitiliza, utumiaji wa madawa ya kulevya na vilevi vingine vinapelekea msanii kushindwa kuwa makini na kazi yake na mwisho wa siku ndio hivyo msanii hupotea.

Hizo ndo sababu zinazosababisha wasanii kushindwa kumaintain kwenye game la muziki wa bongo, pia hizi sababu zikitafutiwa ufumbuzi zitasaidia kukuza wasanii wa muziki vilevile kuwepo ushirikiano baina ya wasanii ili kuondoa mgawanyo wa mashabiki kwa wasanii kutokana na bifu zisizo na msingi ikiwa wote ni wajenzi wa nyumba moja ya bongo fleva.

Endelea kufatilia kurasa zetu kwa story nyingi zaidi. Until next Friday Bye bye.

                                      

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post