Alaaaah!! Niaje mtu wangu karibu kwenye ukurasa wa Smartphone this Wednesday ikiwa ni wiki ya mwisho ya mwezi September.
Leo kwenye kipengele hiki bhana nimeamua kukusogezea njia zitakazo kusaidia kuondoa Password iliyosahaulika.
Je unafahamu unaanzia wapi? Ungana nami kwenye kipengele hiki ili uweze kuwa mjanja zaidi karibu.
Angalizo: Njia hii ni mahususi kwa simu za android pekee, kwani ukifanya hivi katika simu nyingine haitafaa.
- Kwanza kabisa hakikisha umezima simu yako.
- Bonyeza kwa pamoja kitufe cha kuwashia simu (Power Button) na kitufe cha juu cha kuongezea sauti (Volume Up Button) kwa sekunde 5 hadi uone simu inawaka.
- Halafu sasa kwa wale watumiaji wa simu za Samsung Galaxy bonyeza kwa pamoja kitufe cha kuwashia simu (Power Button) na kitufe cha juu cha kuongezea sauti na Home button.
- Kisha bwana utaona maandishi madogo upande wa kushoto yaliyopangwa kushuka chini.
- Bonyeza kitufe cha chini cha sauti ili kuchagua maneno yaliyoandikwa (Wipe data/Factory reset)
- Baada ya hapo bonyeza kitufe cha kuwashia simu (Power Button).
- Acha simu yako ifanye reboot.
- Tayari umefanikiwa kuondoa password au pattern uliyoisahau.
Aaaah weweee!!! Unaonaje njia hizi zilivyorahisi na nyepesi kwako ukijikuta umesahau mtu wangu komaa humu na mambo yatakua fresh kabisaaa this is Smartphone bhanaaa holaaa!!!.
Leave a Reply