Namna ya kuomba kazi nje ya nchi

Namna ya kuomba kazi nje ya nchi

Niaje wanetu sana naeleweka mko njema sana tunakutana tena this weekend kukujuza za ndani kabisa hasa katika segment hii ya kazi, binafsi mimi napendaga fursa bila shaka hata wewe pia unapenda.

Leo bhana katika segment ya kazi tunakusogezea namna ya kuomba kazi nje ya nchi hii nimekusogezea kutokana kwamba watu wengi wamekuwa wakiomba kazi nje na kukwamia njiani au wanaona ugumu wakutuma maombi.

Kitu ambacho mtu unatakiwa kujua katika maswala ya kuomba kazi kila nchi zina utaratibu wake sasa unatakiwa uwe mwangalifu katika hatua hiyo la sivyo unaweza ukakosa kazi sehemu husika au ukaona maombi yake yame kataliwa.

Embu mimi nikushauri mambo unayotakiwa kufanya ukiwa unaomba kazi nje ya nchi yako tena hususani katika mataifa yale yalio endelea kama Marekani.

#Kufikiria juu ya kazi unayotaka kufanya hili ni jambo la kwanza na uandike swali rahisi la kazi katika nchi husika na jina la nchi mfano unaomba kazi ya ukandarasi nchini Uingereza.

#Tafsiri maswali ya kazi utakayo ulizwa unapoanza mchakato katika lugha ya nchi unayotaka kufanya kazi. Hapa tuwekane sawa kwanza unatakiwa ujue lugha ya nchi ambayo unaikusudia kuomba kazi kwasababu itakupa urahisi wa kujua taratibu zao hasa katika nchi za Kiarabu au nchi ya china ambazo lugha zao kidogo unatakiwa uzijue ili uweze kupata ushirikiano

#Google uangalie ni jinsi gani kampuni unayo chagua inaulizaje maswali katika interview tafuta utaratibu wa kazi husika unaweza ukaingia kwenye website mbalimbali uone wengine wanaanda vipi maswali yao ya kazi itakusaidia kurahisisha wa kuandaa maswali yako.

 Na ukiwa unatafuta kazi lazima upitie tovuti mbali mbali mtandaoni uone jinsi gani utapa msaada.

#Chagua nafasi nzuri ambayo inavutia ili ionekane utofauti wa kufanya kazi nje ya nchi na ndani ya nchi kisha unachotakiwa kufanya angalia kama nafasi hiyo kama iko wazi kwa mtu mwenye wasifu wako katika kampuni ulio ichagua huko nje ya nchi.

Iwapo hujui kama una haki ya kufanya kazi rasmi katika nchi hiyo kama wanaitaji wafanya kazi wageni kwa wakati huo.

#Kujua afya yako kwasababu unajianda kwenda ugenini, nchi nyingi zina angalia sana Afya ya mgeni tena husani wewe unaejiandaa kenda kufanya kazi.

Hakikisha umeongea na madaktari wamekufanyia chekup ya mwili mzima yakuwa huna tatizo lolote kutokana kwamba kwenye CV yako wata takakujua ni wapi daktari amehakiki taarifa zako za afya.

Endapo ukakuta unashida katika afya yako ambayo itawaletea shida nchi husika mfano magonjwa ya kuambukiza hapo lazima kuwe naugumu wa kwenda kufanya kazi nje mwanetu.

#Tafuta taarifa za nchi ambayo unatarajia kuomba kazi itakusaidia kujua unaenda kufanya kazi na watu waina gani na ita kupa urahisi wa kuyaelewa mapema mazingira unayotarajia kufanya kazi.

Mbali na hayo unaweza kupata fursa ya ajira kwa haraka kwa kupitia mawakala binafsi wa huduma ya ajira ingawa inachangamoto kidogo kwasababu ukitumia wakala kwa kuomba kazi nje ya nchi ni rahisi laki usipo kuwa makini inaweza ikawa naugumu kwasababu unapoa ajiriwa na nchi nyingine inamaana yule wakala ata julikana yeye ndio amekuleta sasa inapotokea tatizo ni ngumu sana kuji saidia wewe mwenyewe mpaka wakala wako apatikane.

Aidha kuzingatia kuwa katika kutumia fursa za ajira nje ya nchi usalama na haki za msingi ni swala lisilo na mbadala na hivyo nilazima unganishaji wafursa za kuomba kazi uzingatie hapa nawazungumzia mawakala wanao unganisha ajira kutoka nchi mbali mbali wana wajibika kwa kufuata viwango vya kazi za staha vinavyo kubalika nashirika la dunia

Ebanaee!!! Team Scoop inazidi kukuwekea vitu ambavyo vina manufaa kwako najua kunawengi watajifunza kitu kuhusiana uombaji wa kazi huko mbele. wenyewe tunajua ukipata fursa nje ya nchi lazima mchongo uwekweli so usiogope fanya hayo uje kutushukuru baadae mwangu sana sisi Mwananchi Scoop tutakuwa tumekaa pale tuki subiri comment zako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post