Na Christina Joseph
Mambo vipi watu wangu wa nguvu si mnaelewa ule msemo usemao asiyefanya kazi na asili? Basi tufahamu kwamba kazi ni muhimu. Leo kwenye upande wa kazi nimeona tukumbushane kidogo kuhusiana na utafutaji bila kukata tamaa.
Hata kama michongo yako bado haija-’tiki’ au una matatizo yoyote yale ,usikate tamaa mtu wangu kwa sababu muda wako utafika. Katika kukumbushana hilo tumuangalie mwanasheria mtanzania anayeishi Kenya mwenye ulamavu wa mkono lakini hajakata tamaa anapiga kazi zake kama kawa.
Anaitwa David Leonce yeye ni mwanasheria shupavu kabisa kwani licha ya kupata ajali iliyo msababishia kukatwa mkono lakini bado anapiga kazi kama kawa bila kukata tamaa.
David alipata ajali ya barabarani ikampelekea kupoteza mkono wake wa kushoto, hivi sasa anatumia mkono wa bandia uitwao Be bionic ambao humsaidia kushika #Mouse akiwa kazini.
Sasa basi wanangu tujifunze kwa David kwamba no maraa waa hahaaha kila kitu kinawezekana, hutakiwi kukata tamaa, kila changamoto kwako ni fursa na unatakiwa uitumie ili kujipatia kipato, wakati huohuo pia unatakiwa kufahamu kuwa kabla ujafa hujaumbika.
Kwahiyo wale tunaopenda kulala na kukaa vijiweni tuanze kuchakalika tutafute michongo ya kufanya ili mkono uende kinywani. Najua kuna wanangu watakuwa wanajiuliza wapigaje kazi gani wakati hawana elimu au mtaji wa kufanyia biashara.
Sio lazima uwe na elimu kubwa ili uweze kufanikiwa kimaisha, fanya hata biashara kwani sio kila biashara inataka uwe na mamilioni ya pesa, uzuri kupitia jarida letu la #MwananchiScoop sisi sio wachoyo huwa tunakupa mbinu mbalimbali za kibiashara, pitia majarida yetu ya nyuma utajifunza biashara ndogondogo ambazo walaa haziitaji mtaji mkubwa.
Wale wazee wa kuchagua kazi usiruhusu kukaa nyumbani eti kisa unachagua kazi, ukipata mchongo mwanangu upige ilimladi tu uwe mchongo halali ambao hauvunji sheria za nchi na imani yako ya kidini.
Ni hivyo tu watu wangu tupige kazi kama David. Bye byeee hadi Furahii deii nyingine tenaa.
Leave a Reply