Marafiki watakaokuwezesha kufikia malengo

Marafiki watakaokuwezesha kufikia malengo

Katika zama hizi za maendeleo ya kidijitali, ni rahisi sana kufahamiana na watu wengi ambao, hata hivyo, wanaweza wasiwe marafiki wala kuwa na msaada kwako.

Unaweza, kwa mfano, kuwa na ‘marafiki’ hata zaidi ya 10,000 kwenye mitandao ya kijamii, lakini usiwe na rafiki hata mmoja ambaye anaweza kukusaidia kufikia malengo yako.

Marafiki wa kweli na wa karibu ni moja wapo ya mahitaji muhimu sana katika maisha ya mwanadamu jambo ambalo watu wengi hawalifahamu.

Leo kupitia karia tunakufichuliwa siri ya kupata marafiki wa karibu watakaokuwezesha kufikia malengo.

Siri ambayo naifichua ni urafiki na malengo, mara nyingi marafiki zetu tulionao wamekua ni sehemu kubwa sana ya kutufanya einza tufikie au tusifikie malengo tuliojiwekea.

Marafiki ambao watakufanya uweze kufikia malengo yako ya kufanya vizuri darasani, kupiga hatua kwenye biashara ni wale ambao wamekuwa wakikutia moyo pale unapoonekana kukata tamaa.

Pia ni wale watakaokushauri, kukurekebisha wakati unapokosea, kukufariji, kushirikiana na wewe nyakati za huzuni na furaha, kwa hiyo rafiki ana mchango mkubwa katika maisha yako.

Unapaswa kufahamu pia rafiki uliyenaye anayachukuliaje maisha, mafanikio na mambo yako mengine ambayo kwako ni muhimu, kwa kujua hivyo ni rahisi sana kumshirikisha mambo yako na yeye kukushirikisha ya kwake.

Pia hakikisha mara zote rafiki uliyenaye anakusaidia kufanikisha au kuboresha jambo furani la kimaendeleo ambalo unalo na wewe unatakiwa kufanya hivyo hivyo.

Natambua kuwa wapo baadhi ya watu wanashindwa kufikia malengo waliyonayo kwa sababu marafiki walionao ni ukuta wa wao kufanya mambo mazuri na makubwa.

Ni vizuri kuwa makini sana wakati unapochagua marafiki wa kuwa nao karibu na kubadilishana mawazo kila mara, kwani ukipata rafiki mlevi kupindukia, mmbea, mtembezi, mvivu hapo urafiki wenu lazima utatofautiana.

Nasisitiza kuwa kama rafiki uliyenaye ni kikwazo cha wewe kufika pale unapopataka basi ni vizuri ukaachana naye. Kuna wakati unatakiwa kufanya maamuzi magumu ili kuhakikisha kuwa unafikia ndoto zako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post