Mwanamuziki Defao afariki dunia

Mwanamuziki Defao afariki dunia

 

Aiseee!!!moja kati ya stori ambayo imewashtua wengi na kuleta gumzo huko mitandaoni ni hii hapa inayohusu kifo cha Mwimbaji na mtunzi mashuhuri wa Congo Lulendo Matumona maarufu General Defao amefariki dunia.

Defao, alifariki Disemba 27, katika Hospitali ya Laquintinie huko Douala, Cameroon, ambako alikuwa amelazwa hospitalini.

Nikwambie tu kuwa mwimbaji huyo wa Sala Noki atakumbukwa sana kwa sauti yake nzuri na miondoko ya dansi  ambayo ilivutia watu wengi .

Aidha baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo Wanamuziki Ferre Gola na Fally Ipupa walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasilisha salamu zao za rambirambi, wakielezea kifo chake kuwa ni pigo kwa Afrika.

Sambamba na hayo Jenerali Defao aliyezaliwa Kinshasa mnamo Disemba 31, 1958, alianza kuimba mwaka wa 1978 kama sehemu ya Orchester Suka Movema.

 

Pia alicheza kwa muda mfupi na Fogo Stars na Somo West kabla ya kujiunga na Grand Zaiko Wawa na baadaye kuwa sehemu muhimu ya Choc Stars.

Ilikuwa katika kipindi hiki ambapo Defao aliboresha ustadi wake wa uimbaji na uandishi wa nyimbo, akifanya kazi na watu wa nyumbani wakati huo kama Ben Nyamabo na Bozi Boziana.

Defao, katika azma yake ya kujitengenezea nafasi nzuri, aliachana na Choc Stars kuelekea mwisho wa 1990 na kuunda Big Stars na Djo Poster.

Katikati ya miaka ya 90, Defao alikuwa tayari akitishia kufuta majina maarufu kama Koffi Olomide na Bozi Boziana kutoka ulingo wa muziki lakini hakufaulu kupata umaarufu nje ya nchi.

Hata hivyo Defao ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 62 Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu amin.

 

 

 



 

 

 

 

 


 

 

 

 

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post