Mwakinyo afunguka sakata la kuvuliwa mkanda

Mwakinyo afunguka sakata la kuvuliwa mkanda

Bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amefunguka juu ya sakata lake la kuvuliwa mkanda wa Africa Boxing Union (ABU) kwa kuwapa pole mashabiki zake na kusema kuwa malengo yake ni kucheza mikanda mikubwa duniani.

Mwakinyo anayasema hayo baada ya kuibuka kwa taarifa ya kuwa rais wa Africa Boxing Union (ABU) Houcine Houichi amemvua mkanda Mwakinyo kwa kile kinachodaiwa kugoma kupigana na Brandon Tysse kutoka Afrika Kusini kutokana na kukataa ofa ya Dola za Kimarekani 20,000 sawa na Sh. Milioni 46 huku ikidaiwa kuwa mtanzania huyo anahitaji sio chini ya Dola 40,000 sawa na Milioni 92.8.

Mwakinyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ‘‘Poleni sana baadhi ya washabiki mulio shitushwa na taarfa za kuvuliwa mkanda… hio ndio tanzania haonekani ubora na thamani ya unachofanya na ukibatika wata kuongelea vizuri ukiwa umekufa au huwezi tena kufanya ulicho fanya,”

Mwakinyo ameongeza “Ukweli ni kwamba mkanda ni kama zawadi na haina thamani ya kuuza popote ukapata hela kiasi mtu aone nimepata hasara sana kupoteza la hasha ila ina heshima yake kama vikombe kwenye mpira”

”Hili jambo kuna watu wanalielezea kwa namna ya chuki na roho mbaya kwa namna watakavyo wao wakihisi naharibikiwa ila ukweli ni kwamba kwa wasio jua mkanda huo upo kwa ajili ya Africa tu na sio dunia” ameandika

Aidha amesema kuwa hata angekuwa nao hapo alipo leo bado usingekuwa na maana kwake kama hatapigana na wenye rank kubwa zaidi yake.

Amesema kwa sasa focus yake kubwa ni kupata nafasi ya kucheza mikanda mikubwa ya nafasi anazo tamani kufika kidunia.

“Wanao amini watanikatisha tamaa poleni sana mimi sikatishwi tamaa na binaadam mpaka itakapo tokea siku Mungu akafa na mimi utakuwa ndio mwisho wa matumaini yangu lakini sichoki sianguki na sishindwi haijalishi itanichukua muda gani kufika hakuna ane jua kesho yake,” ameandika






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post