Msanii chipukizi Tz ashinda tuzo Kenya

Msanii chipukizi Tz ashinda tuzo Kenya

Msanii Chipukizi na mwanamitindo kutoka nchini Tanzania, Regina Kihwele maarufu kama Gynah ameibuka mshindi wa muigizaji bora kike kwenye tuzo za Lake International Pan African Film Festival (LIPFF).

Tuzo hizo zilizofanyika usiku wa November 6, mwaka huu, nchini Kenya Gynah ambaye pia ni muigizaji amefanikiwa kuwabwaga waigizaji wengine kutoka, Afrika Kusini, Cameroon, Morocco na Uganda.

Gynah ni binti mwenye vipaji vingi aliyeigiza kama muigizaji mkuu katika filamu ya Mulasi iliyompatia ushindi, ambapo aliingiza kama mwanamke jasiri anayebeba machungu mengi ambayo wanawake wengi wakitanzania kwenye ndoa zao huficha.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Gynah amesema tuzo hizo zimekuwa daraja la kukuza sekta ya filamu na utalii ya Tanzania kupitia waigizaji wadogo wadogo wa kike walioshinda.

Gynah kama msanii na mtetezi wa afya ya akili amesema kuwa  anaamini kuwa filamu hiyo ni njia rahisi ya kueneza uelewa kwenye jumuiya ya Tanzania.

“Mimi najiona kama mhamasishaji kwa waigizaji wengine wakike wenye matamanio na pia kuwa kama sehemu ya harakati, hii itanisaidia kufanikiwa kwenye ndoto zangu za kutengeneza filamu za aina ya elimu – burudani kutoka Tanzania,” amesema

Katika tuzo hizo, Tanzania ilikuwa pia kwenye kinyang’anyiro cha muigizaji bora kwa wanaume ambapo msanii Cojack Chilo aliyeigiza kwenye filamu ya “Nyara the kidnapping” aliteuliwa kushindana na wasanii kutoka Ghana, Uganda, Kenya, Afrika Kusini.

Hata hivyo hakufanikiwa kushinda na Rushabiro Raymond kutoka Uganda aliyeigiza filamu iitwayo “Stain” ndiye aliyeshinda tuzo hiyo.

Pia kwenye kikundi cha filamu bora kipengele filamu ya “Nyara the kidnapping” kutoka Tanzania ilikuwa ikishindanishwa na Wateuliwa watatu kutoka Kenya na Uganda na tuzo ilienda kwa filamu ya Mission to rescue kutoka Kenya.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post