- Jenga tabia ya kuyaombea masomo yako kila siku na kila mara, wanafunzi wengi waliofaulu walimweka Mungu mbele kwenye masomo yao.
- Yapende masomo yako na tena uyafurahie.
- Ni vema ukiwa unasoma uwe na Saa, hii itakusaidia kuelewa muda halisi uliosoma.
- Hakikisha unapoanza kusoma uwe umekaa mahali ambapo pana utulivu na hupati usumbufu usio na sababu za msingi.
- Kabla ya kuanza kusoma hakikisha, una kila kitu unachohitaji wakati wa kusoma mfano vitabu, kalamu, karatasi n.k
- Wakati wa kusoma hakikisha unakuwa na daftari jingine ambalo utakuwa unaandika mambo usiyoyafahamu vizuri.
- Kuwa na ratiba yako binafsi inayohusu masomo na uhakikishe unaifuata.
- Tambua ni njia gani ukisoma unaelewa zaidi na ni wakati gani?. Je unaelewa zaidi asubuhi, mchana, jioni, usiku, baada ya kula, kabla ya kuoga, baada ya kufurahi,mitihani inapokaribia n.k
- Epuka makundi mabaya ya wanafunzi wenzio wasiopenda kusoma na watu wanaopenda utani au mizaha, kutojali kuliko kilichowapeleka shule.
- Kuwa na marafiki ambao mtakuwa mmejenga utararatibu wa kuulizana au kuandikiana maswali, kutokana na kile mlichojifunza.
- Ili ufaulu ni lazima uwe na bidii sana katika kusoma, na epuka uvivu.
- Sahau matokeo mabaya uliyoyapata katika mitihani iliyopita
- Ukishasoma, hakikisha unapata mapumziko ya kutosha.
- Kula ni kitu muhimu, hivyo hakikisha umeshiba na sio vema mara umalizapo kula ukaanza kusoma, mimi kama mwalimu wa biology nakushauri pumzika kidogo na jenga
tabia ya kunywa maji mengi, mboga za majani na matunda kwa wingi.
- Jenga tabia ya kufanya mazoezi ya mwili kama vile kucheza mpira, au kuruka kamba n.k
- Tafuta kwa bidii, kujua sababu za wewe kufeli.
- Kaa na wale wanaoweza kile usichokiweza.
- Uliza waliokutangulia hatua walizopitia hadi wakafika walipo, Mfano: unataka kuwa profesa, mtafute Profesa akuelekeze, Daktari mtafute daktari atakupa mwangaza zaidi n.k
- Waheshimu sana wale wote wanaokulea na kukuhudumia kama mwanafunzi.
- Kubali kurekebishwa na kusahihishwa pale unapokosea.
- Ombea mitihani yako kila siku, mpaka umerudishiwa majibu/matokeo yako
- Kumbuka kuwaombea wasahihishaji. Na wao pia ni watu wanachoka na kukosea
- Usifurahi kufeli kwa mwenzako.
- Acha tabia ya kuchagua vipindi vya kuhudhuria darasani wakati masomo yote unatakiwa kuyafanyia mtihani.
- Msikilize mwalimu vizuri anapokuwa anafundisha darasani utafaulu
- Soma maelekezo ya mtihani (instructions) kwa makini
- Usijibu swali bila kuelewa linataka nini?jibu utakalojibu litakuwa tofauti na swali. Hivyo soma swali zaidi ya mara moja ili ulielewe vizuri kabla ya kulijibu.
- Usiwe na haraka ya kumaliza mtihani kwani
kutakufanya usijibu kwa umakini.
- Usiendekeze usingizi katika muda wako wa kujisomea.
- Hakikisha haukati TAMAA.
Leave a Reply